Habari za Punde

Fei Toto Aipeleka Yanga Fainali ya Kombe la Azam Federation Cup.

Rasmi, Klabu ya Yanga Sc yatinga hatua ya fainali kombe la Azam Federation Cup mara baada ya kuwanyuka mahasimu wao Simba Sc kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Bao la Yanga Sc limewekwa kimyani na kiungo matata Feisal Salumu ‘Fei Toto kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango Beno Kakolanya na kutinga fainali.

Yanga Sc sasa wanawasubiri kati ya Azam Fc ama Coastal Unions ambao watauma hapo kesho katika dimba la Amri Abedi Jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.