Habari za Punde

Wazee wa Balaza la CCM Zanzibar Limelaani Kitendo Cha Aliyekuwa Kada wa CCM Mbaraka Shamte.

Na.Is-Haka Omar - Zanzibar.

BARAZA la Wazee wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, limelaani vikali kitendo cha aliyekuwa kada wa Chama hicho Baraka Shamte kutoa lugha zisizofaa na kumkashifu Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kupitia mitanda ya kijamii.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Khadija Jabir Mohamed, wakati akizungumza na waandishi wa Habari hapo Ofisini kwake Kisiwandui Zanzibar.

Alisema Wazee wa Baraza hilo wamesikitishwa na kauli hizo zisizofaa dhidi ya Rais na Serikali hivyo wamekiomba Chama kimchukulie hatua kali za kinidhamu mwanachama huyo.

“Kutokana na lugha chafu alizozitoa, tunakitaka Chama kimchukulie hatua kali dhidi ya uchochezi alioufanya kupitia mitandao ya kijamii.

Wazee tunaamini kuwa hakuna mwanachama yoyote anayeogopwa kuchukuliwa hatua kali kutokana na makosa anayoyafanya”, alieleza Khadija.

Aidha Baraza  hilo limeomba Chama na Serikali wamchunguze kwa kina Baraka Shamte ili kubaini baadhi ya watu waliopo nyuma yake wenye nia ya kuchafua amani na utulivu wa nchi.

Pamoja na hayo Baraza hilo, limesema linaunga mkono hatua za kiutendaji za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi zinazoleta maendeleo ya haraka nchini.

Mapema jana Juni 13,2022 CCM Mkoa wa Mjini kupitia kikao chake cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo imepitisha azimio la kumvua uanachama ndugu Baraka Shamte kufuatia vitendo vyake vya ukiukaji wa maadili ndani ya Chama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.