Habari za Punde

DC TANGA AWAFUNDA WAKUFUNZI WA SENSA NGAZI YA MKOA

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa wa Tanga 381 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Tanga Ufundi Jijini Tanga ambako kulikuwa kunafanyika mafunzo hayo kwa siku 21 kulia ni Katibu Tawala Msaidizi  mkoa wa Tanga Abogust Mmasa

Na Oscar Assenga, TANGA.

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amewataka wakufunzi wa zoezi la Sensa ngazi ya wilaya kutumia mafunzo waliyoyapata kutekeleza jukumu lao kwa ufanisi ikiwemo kujituma kwa bidii na maarifa wakati wa kuwafundisha wasimamizi na makarani ili kuweza kupata matokeo bora ya kazi hiyo ya Kitaifa.

DC Mgandilwa aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa wa Tanga 380 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Tanga Ufundi Jijini Tanga ambako kulikuwa kunafanyika mafunzo hayo kwa siku 21.

 

Alisema katika mafunzo hayo wamejifunza mbinu mbalimbali ikiwemo za kuhoji wakati wakitekeleza majukumu yao hivyo wamewapatia nyenzo sasa kazi kubwa walionayo ni kuifanya kazi kikamilifu na ipasavyo.

“Hivyo lazima mjitume kwa bidii na maarifa wakati wa kutekeleza jukumu lenu la kufundisha wasimamizi na makarani wa Sensa na ndio matumaini yetu ya kupata matokeo bora ya kazi hiyo ya kitaifa”Alisema DC Mgandilwa.

“Sensa katika Mkoa wetu ipo mabegani mwenu mnajukumu la uongozi na dhamana mtakaokuwa mnawafundisha na muwe mfano kwenye nidhamu,kuzingatia muda na ratibu ya mafunzo na mavazi ,lughu ya staha na inayoendena na mafunzo yeyu,mheshimu na kuitendea haki dhamana mliopewa”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema katika Sensa ya mwaka huu wanatakiwa kuonyesha umakini na kuongeza mshikamano haivumilii uzembe wa aina yotote tuwajibike ipasavyo sipendi kuona watu hawatekelezi majukumu yao kwa kutoa visingizo vya hapa na pale.

“Nisisitize kwamba ubora wa mafunzo hayo uwe ubora sambamba na huo mtakaousafirisha kwenye ngazi za wilaya na nimeambiwa mtakapotoka hapa mnakwenda kutengeneza Jeshi nyengine lenye wasimamizi 9527 ambao ndio watatumika kukusanya taarufa za mkoa na hatime kupata takwimu bora za idadi ya watu kwenye mkoa wa Tanga”Alisema

Hata hivyo alisema zoezi la Sensa ni muhimu kwa Taifa kikanda na Kimataifa na litatuwezesha kupata takwimu muhimu zitakazosaidia kupanga,kupima na kutathimini utekelezaji wa mipango yao ya kimaendeleo iwe kisketa na mipango ya kitaifa na kimataifa yatakayogusa kwenye masuala ya kimaendeleo nchini

Awali akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tanga Abogust Mmasa alisema baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo sensa itaongoza mkoa huo ile historia iliyofanyika mwezi wa sita ikifanyika mwezi Agosti mwanzoni itakabidilisha zile takwimu ionekane Tanga watu wanaelewa wanafanya nini.

Alisema wao ni watu wa kutimua vumbi maana yake wao haawavuti mkia wao wanaongoza kwa kila kitu kwa wingi wa Halmashauri na rasilimali zilizopo hiyo hamasa ikifanye kazi kwenye wilaya,kata na vijiji ili kazi ya Sensa iwe na ufinisi na mafanikio.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.