Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Amemuhakikisha Ushirikiano Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Marekani.Mhe Suleiman Haji Suleiman, alipofika Ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo na kumuaga akijitayarisha kwenda Kituo chake cha Kazi Nchini Marekani, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiagana na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.Mhe Suleiman Haji Suleiman, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika kwa mazungumzo na kumuaga akijiandaa kwenda Kituo chake cha Kazi Nchini Marekani.

Na.Abdulrahim Khamis

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemuhakikisha Mashirikiano ya kutosha Naibu Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman. 

Ameyasema hayo katika mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar wakati Balozi huyo alipofika kujitambulisha na kumuaga baada ya kushika Wadhifa huo.

 

Mhe. Hemed amempongeza Balozi Suleiman kwa Imani aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiwakilisha Tanzania ndani ya Umoja wa mataifa ambapo Serikali inategemea mafanikio Zaidi kwa uwakilishi wake.

 

Aidha amemuomba kueleza fursa za uwekezaji zilizopo Nchini na kuwakaribisha Wawekezaji kuja kuwekeza ili kuzidisha Uchumi wa Nchi pamoja kuitangaza Zaidi Tanzania.

 

Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kumuasa Balozi huyo kuitangaza Tanzania kwa mazuri yake hasa Suala la Utalii na vivutio mbali mbali vilivyopo Nchini ili kukuza Sekta ya Utalii Nchini.

 

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amemtaka Balozi Suleiman kueleza Azma ya Serikali kuinua Uchumi wake kupitia Uchumi wa Buluu na fursa zilizomo ndani yake.

 

Nae Naibu Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Suleiman Haji Suleiman amemuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa atasimamia maelekezo aliyopewa na Viongozi Wakuu katika kuiwakilisha Tanzania kwenye majukumu yake ikiwemo kuongeza Diplomasia pamoja na kuzitangaza fursa mbali mbali za kiuchumi zilizopo Nchini.

 

Aidha Balozi Suleiman ameeleza kuwa atakuwa Balozi wa kuitangaza Zanzibar kiutalii kwa kuzingatia Tanzania ina vivutio vingi vya Kitalii hasa Filamu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Royal Tour .

 

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.