Habari za Punde

Benki ya CRDB Kuanzisha Programu ya Uwezeshaji kwa Wajasiriamali Vijana na Wanawake

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kuhusu huduma za kidijitali zinazotolewa na Benki ya CRDB kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki hiyo Michenzani Zanzibar, Ndg.Ahmad Aboubakar (kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja,Wilaya ya Mjini, wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Sita wa Wadau wa Sekta ya TEHEMA unaofanyika katika hoteli  hiyo . Wengine pichani ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (wapili kulia), Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum (watatu kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Benki ya CRDB imetangaza kuanzisha programu ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake wajasiriamali ikiwa na lengo la kukuza ujumuishi wa kiuchumi nchini.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la sita la TEHAMA (TAIC) linalofanyika visiwani Zanzibar kwa muda wa siku tatu kuanzia leo 26 hadi 28 Oktoba 2022.

Kongamano hilo limefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na taasisi kutoka ndani na nje ya nchi.

Nsekela alibainisha kuwa kwa kushirikiana na Tume ya TEHAMA, katika kongamano hilo Benki ya CRDB inakwenda kuzindua programu wezeshi kwa wajasiriamali vijana na wanawake wenye biashara na mawazo bunifu katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta TEHAMA iliyopewa jina la “IMBEJU”.

Benki ya CRDB ni mdhamini mkuu wa Kongamano la TAIC 2022 ambalo limepewa kauli mbiu ya“Mabadiliko ya Kidijitali kwenye Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi”.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa Mkutano katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B” kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Tehama lililofanyika leo 26-10-2022 katika ukumbi wa hoteli hiyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 hadi 28, 2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Tehama Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 hadi 28, 2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajin Nsekela wakati akizungumza na kuelezea huduma za Kidigitali zinazotolewa na benki yake ,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Sita la Sekta ya Tehama Tanzania (kulia kwa Rais) Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania Mhe, Nape Mnauye na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohamed,lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B”.

Viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa wakifutilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la TEHAMA Tanzania,wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Jijini Zanzibar  

Mwakilishi wa UNDP  akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Sita la Sekta ya Tehama Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia  Oktoba 26 hadi 28, 2022.
Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohamed akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 hadi 28, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 hadi 28, 2022.
Viongozi wa Serikali na Wageni waalikwa wakifutilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la TEHAMA Tanzania,wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Jijini Zanzibar  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA nchini, ulioanza leo kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 hadi 28, 2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum iliyotolewa kwa ajili yake, akikapidhiwa kwa pamoja na Mawaziri wa SMT na SMZ, (kulia kwa Rais) Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania Mhe, Nape Mnauye na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohamed, baada ya kulifungua Kongamano la Sita la Tehama Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B”
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi akipokea Tuzo Maalum  kwa nia ya Rais wa Jamhuri wa Muungano Mhe Samia Sulihu Hassan akikabidhiwa na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania Mhe, Nape Mnauye na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohamed, baada ya kulifungua Kongamano la Sita la Tehama Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi “B”

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akielekea katika jukwaa kuu kwa ajili ya kukabidhiwa Cheki cha Udhamini wa Kongamano la Sita la Sekta ya Tehama Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi cheti cha udhamini mkuu wa Mkutano wa Mwaka wa Sekta ya TEHEMA, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huu unaofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar kuanzia leo Oktoba 26 hadi 28, 2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, baada ya kumkabidhi Cheti cha shukrani ya udhamini wa Kongamano la Sita la Sekta ya Tehama Tanzania, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B" kuanzia  Oktoba 26 hadi 28, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.