Habari za Punde

DC Mhe.Kiswaga Vijana Rudini Shamba Kunalipa

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiongea kwenye kipindi cha Morning Talk cha radio Ebony Fm juu ya kuwahimiza vijana kuchangamkia fursa zilizopo kwenye kilimo

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa chama chama mapinduzi Taifa (CCM) amewataka vijana kujikita katika kilimo cha kisasa ambacho ndio mkombozi kwa maisha ya kujiajiri kwa sasa tofauti na kutegemea kuajiliwa serikalini.

Akizungumza kwenye kipindi cha Morning Talk cha radio Ebony Fm,kiswaga alisema kuwa hakuna zao la chakula kwa kipindi hiki ambalo halina soko,kila zao la chakula linasoko kutokana na mahitaji ya kidunia ya sasa.

Kiswaga alisema kuwa wazee wa zamani waliishi na kutajilika kwa kuwa walikuwa wamejikita katika kilimo cha mazao ya Kilimo ambayo yalikuwa yanasaidia kujikimu kwa mahitaji ya familia na kusomesha Watoto wa familia zao.

Hivyo vijana nao wanatakiwa kujikitaka katika kilimo cha kisasa cha mazao ya chakula kwa kutumia teknolojia ambayo itawasaidia wakulima hao kupata masoko kwa haraka kutokana na ubora wa mazao ambayo wanayatoa shambani.

Kiswaga alisema kuwa wakulima wanatakiwa walime wakiwa tayari wameshatafuta masoko kwa sababu hakuna zao ambalo huwezi kukosa soko lakini mkulima anajua namna ya kutafuta masoko ya mazao yao.

Alisema kuwa serikali inatakiwa kutoa elimu ya namna ya kutafuta masoko kwa wakulima kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufanikiwa kuifungua nchi kiuchumi na kuwawezesha watanzania kufanya biashara kila eneo.

"Kwa sasa kila zao la chakula linasoko mfano ukilima mtama,choloko,maharage,karanga na mazao mengine mengi ukilima tu vizuri kwa kufuata teknolojia ya sasa utavuna vizuri na soko utapata hivyo vijana lazima warudi shambani kutafuta mali"alisema Kiswaga

Kiswaga alimazia kwa kusema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefungua nchi kila eneo na wametengezea miundombini mbalimbali ambayo itawawezesha watanzania kufanya shughuli za kimaendeleo hivyo watanzania wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais kwa kazi anayoifanya hivi sasa hapa nchini.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliosikiliza kipindi hicho walisema kuwa wanatakiwa kujikitaka katika kilimo cha kisasa kutokana na mahitaji ya soko la dunia kuhitaji mazao ya chakula kwa wingi kutoka Afrika hususani Tanzania.

Walisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo bado inaardhi kubwa haitumika na yenye rutuba ya kutosha hivyo watanzania wakiitumia vizuri basi watanufaika na kilimo cha kisasa cha mazao ya chakula.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.