Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Rais Felix Tshisekedi Ikulu Zanzibar

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana  na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix        Tshisekedi katika mazungumzo mafupi yaliofanyika Ikulu Zanzibar, mwishoni mwa wiki iliopita.                                                                                                                         

Katika mazungumzo hayo Marais hao walijadili umuhimu wa kuangalia maeneo zaidi ya ushirikiano  kati ya nchi mbili hizo kupitia sekta za kiuchumi na Biashara, wakati huu biashara ya usafirishaji wa Dagaa kutoka Zanzibar kwenda nchini Kongo ikishamiri.

Rais Dk. Mwinyi alimuomba Rais Tshisekedi kuutangaza Utalii wa Zanzibar kwa wadau wa sekta ya Utalii nchini Kongo.

Aidha, Rais Tshisekedi alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kwa mapokezi mazuri aliyopata yeye na ujumbe aliofuatana nao na akatumia fursa hiyo kuahidi kuongeza ushirikiano kati nchi mbili hizo kwa maslahi ya mataifa hayo na wananchi wake.  

Rais Tsisekedi alizuru Tanzania kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili, ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.