Habari za Punde

Mhe Hemed ajumuika na waumini wa Masjid Mukhlisin Potoa kwa Sala ya Ijumaa




Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na Waumini wa Masjid Mukhlisina uliopo Potoa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Akiwasalimia Waumini hao  Baada ya kutekeleza Ibada hiyo Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitamvumilia yoyote atakaejaribu kutoa Taarifa zisizosahihi juu ya Uwepo wa Matendo maovu Nchini.

Ameeleza kumekuwa na Taarifa za Uwepo wa kundi la Vijana linalojinasibu na jina la Panya Rodi ambao huvamia maeneo mbali mbali na kufanya uhalifu.

Aidha Alhajj Hemed ameeleza kuwa Kila Mzazi ana Jukumu la kuchunga Watoto wao kutoingia katika Matendo maovu ambapo Serikali haitokuwa tayari kuona Wananchi wanakosa Amani kwa kuwepo kwa makundi maovu.

"Serikali haitokuwa Tayari kuona Wananchi wanapata shida kwa kundi Dogo la   watu kuanzisha Vurugu" Mhe. Hemed

Sambamba na hayo Alhajj amesema kuwa Serikali inajitahidi kuweka mikakati madhubuti juu ya kuhakikisha Zanzibar inabaki katika Hali ya Usalama ili kurithisha kizazi kijacho kuja kuilinda Amani hiyo.

Pamoja na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameitaka Jamii kuendeleza Mashirikiano baina yao kwa misingi ya Dini ya Uislamu ili kupata Jamii itakayoepukana na Matendo Maovu.

"Tuendeleze Mashirikiano baina yetu katika Jamii ili Watoto wakue katika Misingi ya Dini yetu ambapo watafahamu Mema na Mabaya litaepusha Vijana kujiunga na Makundi Maovu" amesema

Amesema malezi bora yatasaidia kupata Viongozi wenye Maadili Mema  ambao wataweza kuiletea maendeleo Zanzibar.

Akitoa Khutba katika Sala hiyo Imamu Mkuu wa Masjid Mukhlisina  Sheikh Shauri Saleh amewataka Waumini hao kujijenga na Tabia njema na kueleza kuwa Uislamu umehimiza suala la kujijenga na Tabia njema kama alivyo Kiongozi wa Umma huu Mtume Muhammad (S.A.W)

Ameeleza kuwa miongoni mwa sifa ya Waumini wa Kweli ni kuwa na Tabia njema ambazo zitapelekea kutengenea Maisha ya Muumini Duniani na Akhera.

  

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.