MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amesema kwamba serikali
kupitia Wizara ya Afya imeaamua kufanya kampeni ya Chanjo ya Polio na Surua
pamoja na matone ya Vatamin A ili kutokomeza maradhi hayo Zanzibar.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko Masingini Wilaya ya Magharib A Unguja alipozungumza katika
Uzinduzi wa Chanjo ya Surua , Polio na
utoaji wa matone ya Vatamin A kwa watoto kuzuia na kudhibiti mripuko wa maradhi
hayo.
Amesema
kwamba hatua hiyo ya serikali ya kuandesha kampeni ya chanjo hizo ni baada ya
kuwepo mripuko wa maradhi hayo kuanzia
Januari na mwezi Machi mwaka huu ambapo
jumla ya wagonjwa 17,500 wameripotiwa katika visiwa vya Unguja na Pemba .
Aidha Mhe.
Othman amesema kwamba takwimu za hivi karibuni
zinaonesha kwamba kwa kipindi
cha Mwezi Julai hadi Novemba mwaka huu wa 2022 zaidi ya watoto
1,742 wenye umri chini ya miaka 15 wameugua suara na wanane kati ya hao
walifariki dunia.
Hivyo mhe.
Othman amewataka wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanaotoa ushirikiano wa
kutosha kwa kuwapeleka watoto wote wanaopaswa kuchanjwa na kupatiwa matone ya
Viaman A wanapatiwa ili kutokomeza maradhi hayo yanayoweza kusababisha upofu,
kupooza na hata vifo.
Mhe. Othman
amesema kwamba lengo la kampeni hiyo Kitaifa
ni katika jitihada za serikali kuhakikisha inazuia uingiaji wa Ugonjwa wa Plio hapa Zanzibar kulingana na mripuko wa maradhi
hayo uliotolkea katika nchi jirani za Msumbiji
na Malawi.
Hivyo
amesema kwamba wataalamu wa wizara ya Afya watahakikisha kupita nyumba kwa
nyumba katika kampeni hiyo ili kuwachanja na kuwapatia matoni ya vitamin A
watoto wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 350,000 katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Amesema
kwamba serikali inafanya hivyo kwa kuzingatia kwamba kinga ni bora kuliko tiba
na kwamba jitihada hizo zitasaidia kuudhibiti ugonjwa huo na kuutokomeza kabisa
katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha Mhe.
Othma ameutaka uongozi wa wizara ya afaya kuongeza juhudi ya kutoa elimu ya
Afya na uhamasishaji kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hizo kwa kuwa wapo
baadhi ya wananchi wanaendelea kuwa na dhana
mbaya kuhusu chanjo hizo kwa watoto.
Aliitaka
jamii kuthamini kwa vitendo msaada wa chanjo hiyo uliotolewa na Mahrikia ya Kimataifa ili kusaidia kuendesha kampeni
hiyo kwa mafanikio lengo kuu likiwa kulinda afya za watoto wote wa Zanzibar.
Naye Waziri
wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazuri suala la utoaji wa chanjo mbali mbali
liliyumba mnamo mwaka 2020 baada ya kuzuka maradhi ya Kovidi 19 na kwamba baada
ya kudhibitiwa ugonjwa huo nguvu kubwa inaelekezwa katika chanzo za surua,
Polio na utoaji wa matoni ya Vitamin A.
Amewataka
wazanzibari wote wahamasiki na kuitikia wito wa wizara hiyo katika kuhakikisha
watoto wote wanaostahiki kuchanjwa nchi kutote wanapatiwa chanjo hizo kwa
juhudi za pamoja.
Kwa upande
wake Mtalamu wa Chanjo kutoksa Shirika la Afya Duniani (who) Dk. Wilium Mwenge
amesema kwamba Mashirika na wadau mbali mbali wa Afya Duniani , wanaunga mkono
juhudi za serikali za na kwamba kwa pamoja wataendelea kutoa ushirikiano katika
jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.
Chanjo hizo
za surua, polio pamoja na utoaji wa matoni yas Vitamin A imegharamiwa kwa
Pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNISEF), Sherika la
Afya Duniani ( WHO) na shirika la GAVI ambapo shilingi milioni mia nane na
sabiini na sita zimetolewa kugharamia chanjo hiyo .
Mwisho.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Kupitia Kitengo cha Habari leo
tarehe 18.11.202.
No comments:
Post a Comment