Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi mgeni rasmi kongamano la nane (8) la Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) alipofika Hotel ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi leo kufungua kongamano linalohusu maradhi ya Figo.[Picha na Ikulu] 24/11/2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipofuatana na Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) Dr.Onesmo Kisanga (katikati) na  Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (kushoto) mara alipowasili katika Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi kufungua kongamano la nane la Chama hicho lililofanyika leo.[Picha na Ikulu] 24/11/2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam Augustino Mbunda (kushoto) alipokuwa akiangalia vifaa mbali mbali vinavyotumika katika kutibu matatizo ya Figo mara  alipowasili katika Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi kufungua kongamano la nane la Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) lililofanyika leo.[Picha na Ikulu] 24/11/2022. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akiangalia   mashine maalum inayofanya uchunguzi wa matatizo ya magonjwa ya Figo kabla ya  kufungua kongamano la nane la Chama  cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) lililofanyika leo   Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi (kushoto)  Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) Dr.Onesmo Kisanga na Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (kulia kwa Rais).[Picha na Ikulu] 24/11/2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Generics ya Dar es Salaam  inayojishuhulisha na uuzaji wa dawa za figo Bw.Hirak Kumar Sen (katikati) alipotembelea mabanda ya maonesho ya taasisi mbali mbali zinazohusika na uuzaji wa dawa za maradhi hayo kabla  kufungua kongamano la nane la Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) lililofanyika leo.[Picha na Ikulu] 24/11/2022.
Baadhi ya Wataalam  wanaoshuhulika na maradhi ya Figo wakiwa katika kongamano la nane (8) la Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) lililofunguliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo  pichani) katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi leo. [Picha na Ikulu] 24/11/2022.
Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) Dr.Onesmo Kisanga alipokuwa akitoa maelezo ya kina kuhusu Chama chake mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la nane la Chama hicho lililofanyika leo   Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 24/11/2022. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa kufungua kongamano la nane (8)  la Chamacha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) lililofanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi (kulia) Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT) Dr.Onesmo Kisanga,(wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mhe.Hassan Khamis Hafidh na Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui [Picha na Ikulu] 24/11/2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa magonjwa ya  Figo Tanzania (NESOT) Dr.Onesmo Kisanga katika hafla ya  ufunguzi Kongamano la nane (8)  la Chama hicho  lililofanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni,Mkoa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 24/11/2022.    
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.