Habari za Punde

Tanzania Yalishukuru Shirikisho la Judo Ulimwenguni

 

Naibu Katibu Mkuu Said Yakub akizungumza na Rais wa Chama cha Mchezo wa Judo  Nchni  Zaidi Hamisi na kando ni Kaimu Mkurugenzi  wa Maendeleo ya Michezo Nchini Ali Mayay Tembele.)

Na.Adeladius Makwega–WUSM, MJI WA SERIKALI

Serikali imeikipongeza Chama cha Mchezo wa Judo Nchini kwa utendaji wake bora kwani kwa muda mfupi kwani kimefanya mabadiliko makubwa ya utendaji na kusema kuwa serikali itaendelea kuwa nacho bega bega kufanikisha maradufu mafanikio ya mchezo wa huu ili kwenda na dhamira ya serikali ya awamu sita katika kuinua michezo nchini.

Haya yemesema Novemba 30, 2022 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini ndugu Said Yakub wakati alipotembelewa na Rais wa Mchezo wa Judo Nchini ndugu Zaidi Hamisi wizarani hapa Mtumba Mji wa Serikali Jijini Dodoma.

“Mmeainisha mambo mengi ya muda mfupi na ya muda mrefu, jambo la msingi chama cha Judo lazima kiwe taasisi kamili, yenye mipango ya muda mrefu, muwe na mpango mkakati wa miaka mitano, muwe na kituo cha mafunzo, hapo litakuwa eneo ambalo mafunzo ya mchezo huo yatafanyika. Serikali itaratibu ufundishaji wa Judo mashuleni kwa ushirikiano na wizara zinazosimamia shule zetu. Tunamshukuru Rais wa Shirikisho la Judo Ulimwenguni Ndugu Marlus Vizer kwa kutoa msaada wake kwa michezo huo na tunamualika aje Tanzania kukutana na viongozi wa michezo nchini.”

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Yakub alipigia chapuo Chama cha Mchezo wa Judo kupewa vyumba vya kuchezea mchezo huo katika viwanja vyetu vya michezo nchini, hilo alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Ndugu Ali Mayay Tembele kulitekeleza.

Akizungumza katika kikao hicho Rais wa Mchezo wa huo ndugu Hamisi alipokea pongezi hizo kwa mikono miwili akisema kuwa Tanzania itapokea jozi 50 ya nguo za mchezo wa judo katika mashindano ya kimataifa, jozi 100 za nguo za mafunzo ya mchezo huo na pia jozi 200 za nguo mazoezi kwa ajili ya wanafunzi na pia Tanzania itapata nafasi ya kusomeshewa walimu wa mchezo huo kwa ngazi ya shahada.

Judo ni mchezo wenye asili ya Japan huku ukichezwa sana katika mataifa ya Bara Ulaya ikiwamo Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.