Habari za Punde

mashindano ya mbio za marathon zinazojuilikana RUN4BINT zilizofanyika katika manispaa ya Mjini Unguja,

Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (katikati) na Waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui pamoja na Viongozi mbali mbali na Wananchi wakishiriki katika   matembezi ya Kilomita tano yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community Chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg,Flora Njelekela (wa tatu kushoto)   kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar

Na Maulid Yussuf WMJJWW

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi amesema suala la ukosefu wa bidhaa na uelewa juu ya hedhi ni changamoto kubwa nchini ambapo watoto wa kike wanakosa masomo kwa siku 3 hadi 7  wanapokuwa kwenye siku zao.

Akisoma hotuba kwa niaba yake baada ya mashindano ya mbio za marathon zinazojuilikana RUN4BINT zilizofanyika katika manispaa ya Mjini Unguja, Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kupatwa na maumivu makali wakati wanapokuwa katika siku zao.

Katika hotuba hiyo Maryam ametoa wito kwa wadau wa maendeleo na wanaotetea haki za mtoto wa kike kuhakikisha kwamba watoto wa kike wanapata bidhaa hizo ili waweze kupata haki yao ya elimu kwa kuhudhuria vipindi kwa uhuru pale wawapo kwenye hedhi kama watoto wa kiume na kusisitiza kuchukuliwa suala hilo kuwa ni la dharura kama lilivyokuwa suala la madawati.

Mama Maryam pia ametoa rai kwa Wahusika wote katika usimamizi wa Elimu na Afya kuandaa mkakati wa makusudi utakaojielekeza kutatua changamoto hizo na  kuangaliwa kwa umuhimu wake pamoja na kubuni jitihada za makusudi ili kuondoa kabisa changamoto hizo kwa kujenga mazingira wezeshi kwa wanafunzi wa kike. 
 
Amesema Serikali na wadau wengine wanaendelea kufanya juhudi mbali mbali katika kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanasoma wakiwa katika mazingira raifiki na yenye kushajihisha upatikanaji wa masomo yao ya kila siku ili kufikia ndoto zao za msingi. 

Pia mama Maryam ameshauri kuwa  zoezi hili kutoishia hapa na badala yake liendelee kuratibiwa kwa kadiri ya mahitaji kwa kuwa bado kunachangamoto nyingi ambazo watoto wa kike wanapitia na zaidi kuangalia maeneo yote ya nchi, mijini na vijijini. 

Pia amewanasihi wadau wote kuendelea kuekeza kwa watoto wa kike ili kuwaepusha na changamoto wanazoweza kuzipitia na kutimiza wajibu huo na sio kuwapendelea watoto wakike bali ni kuwatimiza mahitaji na haki zao za msingi za kimaumbile ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii, kiuchumi na kielimu. 

Katika hituba hiyo pia Mama Maryam ameelezea kufarajika kwake kuona kwamba wapo watu waliokimbia kilomita 5, 10 na wapo ambao hawakukimbia lakini wameungana nao katika kuhakikisha kuwa huduma za vifaa hivyo zinapatikana kwa kutumia michango yao na kuwashukuru kwa moyo huo kwani kutoa ni moyo na sio utajiri.

"Tuendelee kuungana kwa pamoja katika kuimarisha ukombozi wa mtoto wa kike na hata wa kiume ili kusimamia maslahi yao kwa ujumla" amesisitiza mama Maryam 

Amesema upatikanaji wa vifaa hivyo utachochea ushiriki  mzuri wa watoto wa kike katika shughuli za masomo na makuzi yao pamoja na shughuli za maendeleo katika ngazi ya Familia na  Jamii.

Nae Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewashukuru wa wananchi wote walioshiriki katika mbio hizo kwa namna moja au nyengine pamoja n kuwashukuru kwa upekee mawaziri mbalimbali walioungana nao katika mbio hizo.

Pia ametoa pongezi kwa uongozi wa Taasisi ya Smile for Community  kwa kuratibu mashindano hayo yenye lengo la kuwasaidia na kutatua changamoto zinazowakabili watoto wa kike maskulini.

Mpema Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Smile for Community bi Flora Njelekela  amesema lengo la kufanya mbio hizo ni kusaidia upatikanaji wa fesha kwa ajili ya kununua vifaa vya hedhi zikiwemo Taula za kike, nguo za ndani, sabuni pamoja na mahitaji mengine, ili kumsaidia aweze kuhudhuria masomo yake kama kawaida.

Amesema kumekuwepo matatizo mengi yanawapata watoto wa kike wanapokuwa katika siku zao kwa kukosa bidhaa za hedhi, maji safi, vyumba maalum vya wasichana na hata mabweni hali inayowafanya wengine  kutohudhuria skuli.

Hivyo amewaomba wananchi kushirikiana pamoja kutatua changamoto hizo zinazowakabili watoto wa kike maskulini ili kuwajengea mustakbali mzuri wa maisha yao.


Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi akifyatua bastola kama ishara ya kuzindua  mbio za kilomita kumi samba na kilomita tano wakiwemo na watu wenye ulemavu na pamona na matembezi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi akifyatua bastola kama ishara ya kuzindua  mbio za kilomita kumi samba na kilomita tano wakiwemo na watu wenye ulemavu na pamona na matembezi yaliyotayarishwa na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (katikati) akijumuika na wananchi mbali mbai na Viongozi walioshiriki   katika   matembezi ya Kilomita tano  kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar,ambapo Taasisi ya Smile for Community Chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg,Flora Njelekela (wa pili kushoto) imetayarisha matembezi hayo pamoja na mbio za Kilomita kumi,tano wakiwemo na Watu wenye Ulemavu tafauti 
Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akivalishwa nishani na   Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Smile for Community Ndg. Flora Njelekela mara baada ya kumalizika kwa  matembezi kilomita tano,mbio Kilomita tano na kumi yaliyotayarishwa  na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar pia  Mwenyekiti wa  Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma (kulia) mara baada ya kumalizika kwa  matembezi kilomita tano yaliyofanyika leo sambamba  na mbio Kilomita tano na kumi hafla iliyotayarishwa  na Taasisi ya Smile for Community kuanzia Ngome Konge,Mlandege hadi Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 03/12/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.