Habari za Punde

Michuano ya 17 Kombe la Mapinduzi Zanzibar Kati ya Malindi na Azam Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan.Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao. 1-1

Mchezaji wa Timu ya Azan na Malindi wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja leo jioni.Timu hizo zimetoka sare ya Bao 1-1.

Michezo wa Malindi na Azam uliofanyika jioni hii Timu hizo zimeshindwa kuoneshana ubabe na kutoka suluhu ya bao 1-1.

Timu ya Azam ilikuwa ya kwanza kuona lango la Timu ya Malindi katika dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza mshambuliaji ya Azam Ayubu Lyanga ameipatika bao timu yake 

Wachezaji wa Timu ya Malindi kipindi cha pili cha mchezo huo walikuja na nguvu mpya na kulishambulia lango la Azam na katika dakika ya 77 ya mchezo huo kipindi cha pili mshambuliaji Timu ya Malindi Said Omar aliipatika timu yake bao la kusawazisha.
Timu ya Malindi katika mchezo huo walipata uhai katika dakika za mwisho za mchezo kwa washambuliaji wake kupoteza nafasi za kufunga hadi mwisho ya mchezo huo.
Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.