Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wasanii
wa Wasafi, kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuburudisha na kuihamasisha jamii.
Dk. Mwinyi alitoa
pongezi hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na msanii Mbwana Yussufu maarufu Mbosso
aliyefika hapo kwa mazungumzo.
Rais Mwinyi alisema
wasanii ni kiungo chenye kufikisha ujumbe haraka kwa hadhira kutokana na mvuto
mkubwa kwa jamii.
Aliwashukuru wasanii
hao kwa utayari wao wanaoutoa nata kwenye sherehe za chama na Serikali kwa kazi
kubwa ya buirudani jamii.
Naye, Msanii huyo
aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango mkubwa inayowapa
wasanii Tanzania.
Aliiahidi Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana nayo hasa kwenye masuala ya kijamii na
kuwaeleza muda wote yupo tayari kulitumika taifa.
Alimueleza Dk.
Mwinyi ujiuo wake kwa Zanzibar mbali na kufanyakazi kwa mashabiki wake lakini kupata
baraka kwa viongozi wa Serikali na kumueleza Raisi kwamba yupo tayari kuchangia
kwenye sekta ya maendeleo wakati wote.
Aidha, Mbosso alitumia
fursa hiyo kumueleza Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa taasisi
ya Maisha bora Foundation, Mama Maryam Mwinyi, kwamba yupo tayari kushirikiana
na taasisi hiyo katika harakati za kuitumikia jamii kwa maendeleo.
Alisema Zanzibar ana
mashabiki wengi wa muziki wake na kueleza ameamua kuufungua mwaka kivyengine
Zanzibar na kuwaahidi mashabiki wake hushuhudia makubwa kwa aliyowatayarishia.
Akiwasilisha salamu
za Mkurugenzi wa Wasafi Media, Abul Naseeb maarufu Diamond Platinum mbele ya
Rais Mwinyi, Mkuu wa Idara ya Habari ya Wasafi media, Stancer Lameck alimueleza
Dk. Mwinyi kwamba daima Wasafi wanaungamkono juhudi anazozifanya za kuifungua
nchi kimaendeleo.
Alisema Diamond
anaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwafungulia
milango ya fursa Wasafi na kuahidi watakua mabalozi wazuri wa kuitangaza
Zanzibar kimataifa kupitia utalii.
Mbosso alianza
muziki tokea akiwa na kundi la Yamoto wakati huo akitambulika kwa jina la
Maramboso mnamo miaka 2013 kabla ya kusambaratika kwa kundi hilo kwenye miaka
ya 2015 na baadae mwaka 2018 alifunga mkataba na kampuni ya WCB ya Wasafi
ambako aliendeleza safari ya muziki wake.
Miaka miwili
iliyopita nyota huyo wa muziki wa solo, bongo flava, mtunzi wa nyimbo na mpiga gitaa,
Mosso alifanikiwa kupata mashabiki wengi zaidi kwenye kurasa zake za mitandao
kwa wakati huo alifanikiwa kutimiza zaidi ya mashabiki milioni moja kwenye
mtandao wake wa “yutube” .
Mwaka 2021
alifaikiwa kuiteka hadhira ya mashabiki wake kwa wimbo wake wa “Maana ya
Mapenzi” (Definition of Love) aliyowashirikisha wasanii nguli wa bongo fleva
akiwemo bosi wake, Diamond Platinum,
kundi la Njenje, Msanii maarufu kutoka Nigeria, Mr. Flavaur, Rayvanny,
Liya, Daraaasa, Baba Levo na Diana.
IDARA YA MAWASILIANO,
IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment