Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar
imetwaa ubingwa katika mchezo wa kirafiki wa kuadhimisha siku ya sheria Zanzibar
baada ya kupata ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu ya Mahkama.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Mao Zendong
watunga sheria hao wa Baraza la Wawakilishi waliovalia jezi za kijani waliweza
kuonesha soka safi na kuwafanya wapinzani wao kuruhusu magoli matatu ya papo
kwa papo ambayo yalisimama hadi kumalizika kipindi cha kwanza.
Timu ya Mahkama walikianza kwa kasi kipindi
cha pili na kufanikiwa kurudisha magoli mawili ambapo hadi mwamuzi wa kati
anapuuliza kifirimbi cha kumaliza mchezo huo timu ya BLW walikuWa mbele kwa
goli 3 – 2.
Ushindi huo umeendeleza mwendo mzuri wa timu
ya watunga sheria hao kwa kucheza michezo ya mashindano mbali mbali bila
ya kupoteza.
Viongozi wa timu zote mbili za baraza la
wawakilishi na mahkama wakauelezea mchezo huo pamoja na mipango yao katika
kuzinoa timu zao ili ziweze kuwa bora zaidi.
No comments:
Post a Comment