Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amewaapisha Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj.Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa na wa Afrika Mashariki katika hafla ya Kuapishwa Makamishana wa Tume ya Utumishi wa Umaa leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Makamishna wawili wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.                                                                                                     

Walioapishwa ni Ndg. Yakout Hassan Yakout na Ndg. Asha Khamis Hamad kuwa Makamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.

Ghafla hiyo ilifanyika Ikulu, Zanzibar imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdallah, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dk. Mwinyi Talib Haji, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi, Zena Ahmed Said, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrisa Mustafa Kitwana.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Jamal Kassim Ali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Msatahiki Meya wa jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Mussa, Viongozi wa dini pamoja na familia.

IDARA YA MAWASILIANO

IKULU,ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj .DK. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bw.Yakout Hassan Yakout kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar
Bw.Yakout Hassan Yakout akila kiapo mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kuwa   Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bi.Asha Khamis Hamad  kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar.
Bi.Asha Khamis Hamad akila kiapo mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kuwa   Kamishna wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.