SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeahidi kwamba itashughulikia Changamoto za wakaazi wa Kijiji cha Bumbwini Kiyongwe za ukosefu baadhi ya huduma muhimu za kijamii zinazowakabili ili kuleta ustawi bora wa maendeleo ya Kijamii.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.
Othman Masoud Othman, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Cahama cha ACT-
Wazalendo Zanzibar, ameeleza hayo huko Bumbwini kiyongwe Kaskazni B Unguja akiwa
katika mfululizo wa ziara za kuwakagua
na kuwafariji wangonjwa na wananchi waliopatwa na misiba katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema kwamba serikali imepokea
kutoka kwa wananchi na kuona kuwepo kero kubwa ya ukosefu wa usafari wa
barabara jambo linalochangia kodhoofisha
shughuli za kimaendeleo kwa wananchi wanaoishi kwenye kijiji hicho.
Mhe. Othman amesema kwamba kero kubwa ya
barabara, iliyopo inayochangia wahudumu wa afya na waalimu kutofika na kurudi
kwa wakati katika vituo vyao vya kazi ndani ya kijiji hicho na kwamba suala
hilo kero ambayo serikali italishughulikia na kulipatia ufumbuzi.
Kwa upande mwengine Mhe. Othman
aliwaleza Viongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo katika ngazi ya wilaya na Mikoa
kuiga mfano wa wenzao wa mjini kuanzisha mifuko ya faraja itakayotumika
kusaidia kutatua changamoto mbali mbali walizonazo wananchi kwenye maeneo yao.
Aidha amewaka viongozi hao pia
kuendeleza ziara katika majimbo yao ili
kuonana na kupokea changamoto mbali mbali zilizomo kwenye maeneo tofauti na
kwamba kufanya hivyo ndio wajibu muhimu wa kiongozi kuwatumikia wananchi.
Mapema wakaazi wa Kijiji cha Kiyongwe
walimueleza Mhe. Othman kwamba Kijiji hicho hakina barabara kwa muda mrefu sasa
jambo linalochangia wananchi kupata shida ya kuingia na kutoka katika kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo
za kila siku huku wahudumu wa afya na walimu wa skuli hiyo ikidhoofisha
utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha wananchi hao walimueleza Mhe.
Makamu kwamba kero kubwa ya barabara
iliyopo katika kijiji hicho inachangia walimu pamoja na wahudumu wa Kituo cha
Afya cha Kijiji cha Kiyongwe Kidogo kushindwa kufika kazini kwa wakati ili
kuwahudumia wananchi kama inavyohitajika.
Wamesema kwemba wafanyakazi hao
wanalazimika kukodi boda boda kila siku ili
kuweza kuingia na kutoka kazini ama kutembea masafa marefu kwa miguu jambo
ambalo linachangia kupunguza ufanisi wa shughuli za utekelezaji wa majukumu ya wafanyakazi hao kila siku.
Mhe. Othman katika ziara hiyo
alitembelea katika Majimbo Bumbwini, Donge, Tumbatu, Nungwi , Mkwajuni, Kiwengwa , Kijini ,
Chaani pamoja na Mahonda kuwakagua wagonjwa na watu waliofikwa na msiba ikiwa
ni mfululizo wa kuendeleza ziara zilizokuwa zikifanywa na mtangulizi wake marehem
Maaalim Seif Sharifu Hamad na kwamba ziara hiyo kesho itaendelea katika Mkoa wa
Kusini Unguja.
MWISHO
Imetolewa Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe 27.03.2023.
No comments:
Post a Comment