RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al
hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii kwa kila mwenye uwezo kuendelea
kuwasaidia wenye uhitaji ili kupata fadhila za mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Al- hajj Dk. Mwinyi
aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi walio kwenye makundi maalumu
wakiwemo wazee, wajane, watoto yatima na wenye ulemavu huko viwanja wa
Mapinduzi Square, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan ni mwezi wa neema na inampendeza Mola, watu wote kuishi kwa upendo,
ushirikiano na kusaidiana hasa kwa jamii zenye uhitaji zisaidiwe kwa kadri ya
uwezo watu waliojaaliwa nao.
Alisema msaada wa
vyakula uliotolewa na taasisi ya Maendeleo ya “Zanzibar International
Development Organization” umekuja wakati jamii unauhitaji, hivyo, Rais Dk.
Mwinyi aliendelea kutoa wito kwa wadau wengine na wananchi wenye uwezo
kuendeleza moyo wa kuwasaidia wengine wenye uhitaji ili kujenga jamii yenye
kumpendezesha Mwenyezi Mungu.
“Chakula hiki kuwapa
watu wasiokua na uwezo, Mwenyezi Mungu awalipe pepo ndegu zetu wafadhili hawa”
Dk. Mwinyi aliwaombea Kheri wafadhili waliotoa msaada huo wa vyakula kwa
makundi maalum.
Aidha, Rais Mwinyi,
aliishukuru taasisi ya maendeleo ya “Zanzibar International Development
Organization” ambao walijitolea kutoa msaada huo wa vyakula na mahitaji mengine
kwa jamii hio.
Akizungumza kwenye hafla
hiyo, mmoja wa wanufaika wa sadaka hiyo, Jamila Boraafya (Mwenye ulemavu wa
kuona) alimshururu Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada anayoichukua kuwafikia wananchi
wake wa makundi yote.
Alisema uongozi wake
umekua mfano wa kuigwa wa viongozi wengine wa ngazi zote katika kuwahudumia
wanaowangoza.
“Tunakushukuru sana Mhe.
Rais Dk. Mwinyi, juhudi zako tunaziona na upendo wako kwetu wananchi wako,
hakika wewe ni kiongozi wa mfano na Mwenyezi Mungu ataendelea kukulipa mema kwa
kututumikia, unafika hadi mataifa ya nje kwaajili ya kutuhangaikia sisi wananchi
wako, ahsate sana na Mola azidi kukulipa kheri” alishukuru Jamila.
Zoezi kama hilo la
ugawaji wa sadaka ya iftari kwa mwezi huu mtukufu Ramadhan, Rais Dk. Mwinyi pia
alilifanya kwa Wilaya nne za Pemba kwa mikoa yote ya Kusini na Kaskazini wakati
wa ziara yake ya siku mbili kisiwani himo, iliyomalizika hivi karibuni.
IDARA
YAMAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment