Habari za Punde

Wafanyakazi wa Benki ya NMB Wajumuika na Wateja Wao wa Zanzibar Katika Iftari Maalum Iliyoandaliwa kwa Ajili yao

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Watendaji Wakuu wa Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB Bw.Benedicto Baragomwa (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B" Unguja kuhudhuria hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Wateja wake. 
Afisa Mkuu wa Biashara na Serikali wa benki ya NMB.Bi. Vicky Bishubo akijumuika na Wananchi na Wateja wa Benki ya NMB Zanzibar katika Iftari iliyoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B" Unguja, iftari hiyo imekwenda sambamba na Miaka 25 ya NMB. 
Wananchi na Wateja wa Benki ya NMB wakijumuika katika Iftari Maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa Wateja wao wa Unguja, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi "B" Unguja. 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.