Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokua akitoa taarifa kuhusiana na Mkutano wa kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unaotarajiwa kuanza Mei, 10, 2023 huko Chukwani Zanzibar.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akizungumza na Waandishi wa Habari wakati alipokua akitoa taarifa kuhusiana na Mkutano wa kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unaotarajiwa kuanza Mei, 10, 2023 huko Chukwani Zanzibar.
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.
Mkutano wa kumi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 10 Mei, 2023, saa 3:00 asubuhi ambapo maswali 246 yameratibiwa kwa ajili ya mkutano huo.
Akito taarifa kuhusu shughuli zitakazofanyika katika mkutano huo huko Chukwani Katibu wa Baraza hilo Raya Issa Mselem amesema kuwa Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu maswali hayo na kujadili bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha amefahamisha kuwa katika mkutano huo jumla ya miswada minne ya Sheria itawasilishwa na kujadiliwa.
akielezea baadhi ya miswada hiyo itakayowasilishwa na kujadiliwa Katibu Raya alifahamisha kuwa ni pamoja na Mswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill) , Mswada wa Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2023/2024,na Mswada wa Kufuta Sheria ya Kuzuiya Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar Nam. 1 ya Mwaka 2012 na Kutunga Upya Sheria hiyo .
Aidha Katibu Raya ameongeza kwa kusema kuwa Sheria ya Kuanzisha Shirika la Mawasiliano Zanzibar na Kuweka Masharti Yanayohusiana na Huduma ya Miundombinu ya Tehama itajadiliwa.
Pia Katibu Raya amesema miswada ya kusomwa kwa mara ya kwanza itawasilishwa na kujadiliwa katika kikao hicho.
No comments:
Post a Comment