Na Khadija Khamis, Maelezo, 30/07/2023 .
Meya wa Jiji la Zanzibar,Mhe. Mahmoud Mohamed Mussa amesema Kampuni ya Edmark itawasaidia vijana kujipatia ajira kuepukana na kujiingiza katika vitendo viovu vya kutumia madawa ya kulevya.
Hayo ameyasema huko Mombasa katika Kampuni ya Edmark wakati wa sherehe ya kutimiza miaka mitatu tangu kufungua kwa Tawi lake hapa Zanzibar huko Ofisini kwao Mombasa Wilaya ya Magharibi 'B'..
Amesema kwamba iwapo vijana watakidhi vigezo vyao wawasaidie kuwachukuwa ili kujipatia ajira na kujiepusha kukaa vijiweni ambako kunavishawishi vya aina mbali mbali ikiwemo kujiingiza katika uraibu wa madawa ya kulevya .
Aidha alifahamisha kuwa serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hazikubaliani na mambo ya jinsia moja aliwataka wazazi na walezi kuwaelimisha vijana wao ili wasijiingize katika mlolongo wa mambo hayo .
Meya Mahmoud akizungumzia suala zima la udhalilishaji na kuwataka akibaba kujitahidi kuwatunza akinamama na watoto ili kuwe naTaifa lililobora nchini .
“Tujitahidi kuwalinda na kuwasaidia watoto wetu kwani watoto tulionao ndio taifa letu la kesho ,” alisema Meya Mohmoud .
Alieleza kuwa kwa taarifa alizopokea kutoka Ofisi ya Mufti talaka zimekuwa nyingi jambo ambalo linachangia mmon’gonyoko wa maadili hivyo aliitaka jamii kujitahidi kuzidumisha ndoa zao ili mambo yawe sawia.
Vile vile aliiyomba kampuni hiyo kuyaendeleza yale mazuri ambayo wanania ya kuyafanya ili iwe chachu ya kuwasaidia wazanzibar na watanzania kwa ujumla na Serikali ipo pamoja nao ili kuhakikisha kunaondokana na changamoto zilizopo na kuijenga Zanzibar yenye umoja mshikamano kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Nae Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Edmark Ms Maylyn alisema hivi karibuni watazindua bidhaa zao mpya ambazo zitawasaidia watu wenye changamoto ya macho.
Aidha alisema bidhaa yao ya splina liquid ya kusawazisha mmengenyo wa chakula katika mtumbo mpana wanatarajia kuzileta za vidonge ili kurahisisha uchukuaji wa wateja wanaosafiri nje ya nchi .
Kwa upande wa Dr Salma Chande kutoka Tanzania Bara akitoa elimu kwa wanachama hao alisema kuwa saratani ya utumbo mpana ni gonjwa namba moja kwa kuua watu katika karne ya 21.
Aliiyomba jamii kuacha ulaji wa chakula cha uwanga katika nyakati za usiku kwani ni hatari kwa afya zao aliwataka kutumia matunda na mboga mboga kwani wakati wa kulala hakuna mmengenyo wa vyakula ila vyakula vyote hugeuzwa kuwa mafuta .
Aidha alisema dalili kuu ya magonjwa sugu huanza tumboni bacteria humengenya na kuzalisha sumu za aina tatu na kiwango kikubwa cha tendikali kinasababisha uzee wa mapema na unene wa kupitiliza .
No comments:
Post a Comment