Habari za Punde

*Viongozi wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Waendelea Kupata Uzoefu wa Mageuzi ya Utendaji*

Na Shamimu Nyaki

Viongozi na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo  wameendelea kupokea elimu kupitia Mada mbalimbali zinazotolewa na viongozi na Wataalam mbalimbali katika nyanja tofauti katika Kikao cha Faragha cha siku tatu cha viongozi hao kinachoendelea Mkoani Morogoro.

Viongozi hao chini ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu wamepokea Mada kuhusu  Itifaki na Ustaarabu iliyowasilishwa na Bw. Batholomeo Jungu, Mkurugenzi wa Maadhimisho kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mada kuhusu  Rasilimaliwatu kama dhamana ya Taasisi iliyowasilishwa na Bw. Daniel Materu.

Maada nyingine ni Mabadiliko ya Kitaasisi kupitia uzoefu wa NSSF  iliyowasilishwa na Mhe. Balozi Dkt. Ramadhan Kitwana Dau pamoja na Mada ya Tatizo letu  ni nini dhidi ya matarajio yetu iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu.

Aidha, Viongozi hao pia walipokea Mada kuhusu Sifa ya Uongozi katika ulimwengu wa kisiasa iliyowasilishwa na Bw. Daniel Materu, ambapo walipata nafasi ya kuzijadili, kuuliza maswali, kutoa maoni, ushauri na kupata  ufafanuzi wa maswala mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.