PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO
Na Fauzia Mussa Maelezo
Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ZFDA imeteketeza jumla ya tani 15 za vifaa tiba na vipodozi visivyofaa kwa matumizi ya Binaadamu.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo huko Kikungwi,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Dawa na Vipodozi ZFDA Haji Juma Khamis amesema baadhi ya bidhaa katika mzigo huo zilipitwa na muda wa matumizi zikiwa sokoni na baadhi ziliingizwa Nchini Kinyume na utaratibu.
Alisema ZFDA ina jukumu la kumlinda mtumiaji hivyo mara tu wanapobaini bidhaa zilizopoteza ubora huzuia na kuzifanyia uteketezaji bidhaa hizo endapo hakuna uwezekano wa kurudishwa zilikotoka.
Alifahamisha kuwa ZFDA huteketeza vifaa tiba na vipodozi kwa kuzichoma moto kutokana na kukosa mashine maalum za kuangamizia bidhaa hizo kwa muda mfupi na kwa urahisi zaidi.
Hata hivyo Aliwashauri wafanyabiashara kuingiza bidhaa kwa kuzingatia muda wa kuishi na kuwataka kuagiza mzigo kulingana na mahitaji ya soko ili kuepusha hasara zisizotarajiwa.
No comments:
Post a Comment