Habari za Punde

DUA KATIKA KABURI LA SHEIKH THABIT KOMBO YAFANYIKA ZANZIBAR

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga (mwenye koti) akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika Dua kwenye kaburi la aliekuwa Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo Ikiwa ni Muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,hafla iliofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga akizungumza na Wananchi na wanafamilia baada ya kumaliza  Dua kwenye kaburi la aliekuwa Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo Ikiwa ni Muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,hafla iliofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhan Soraga akitoa Sadaka kwa kiongozi wa Familia kuonesha Mapenzi na Mshikamano baada ya kumaliza  Dua kwenye kaburi la aliekuwa Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo Ikiwa ni Muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,hafla iliofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Kiongozi wa Familia Muhidini Muhsin Ali akitoa neno la Shukurani baada ya kumaliza  Dua kwenye kaburi la aliekuwa Katibu wa Kwanza wa Chama Cha Afro Shirazi Marehemu Sheikh Thabit Kombo Ikiwa ni Muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa,hafla iliofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja.

Na. Khadija Khamis –Maelezo. 03/04/2024.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inatambuwa Mchango Mkubwa uliotolewa na Waasisi wa Mapinduzi katika kujenga Nchi na kuiletea Maendeleo.

 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameyasema hayo wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Sheikh Thabit Kombo Jecha, aliekuwa katibu mkuu wa kwanza wa Chama cha Afro shirazi huko Chukwani, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya kuwaenzi viongozi wa kitaifa.


Amesema Marehemu Sheikh Thabiti Kombo alikuwa mpatanishaji

na mtulizaji wa Taharuki kwa Rais wa awamu ya kwanza wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume pamoja na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere katika suala zima la kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

Aidha ameeleza alikuwa ni mwalimu wa kutoa taaluma kwa jamii na kutoa busara kubwa wakati wa vuguvugu la muungano na umuhimu wa kudumisha muungano na ustawi wa taifa.


“Marehemu alihakikisha analisimamia taifa letu kwa uzalendo na kuiletea maendeleo kwani alikuwa na uzalendo na mapenzi ya nchi yetu,” amesema waziri Soraga


Amesema mengi aliyoyaacha imekuwa mfano bora kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo hivyo hakuna budi kuaenzi na kuayendeleza kwa maslahi mapana ya Taifa.


Akitoa neno la shukurani Mwakilishi wa Familia ya Marehemu, ndg. Muhidin Muhsin Ali ameishukuru Serikali kwa kusimamia na kuendeleza suala la kumtakia dua ya kheri na uwadilifu mzee wao huyo.


Marehemu Sheikhe Thabit Kombo Jecha amefariki Agasti 28 Mwaka 1986 na kuzikwa kijijini kwao Chukwani Wilaya ya Magharibi ‘‘B’’, akiwa na umri wa miaka 82.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.