Habari za Punde

Makatibu wa UWT Wapongezwa kwa kuhamasisha Wanachama kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili wa kadi za CCM kwa mfumo wa Kieletroniki

Na Takdir Ali. Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Magharibi kichama Mhe. Amina Iddi Mabrouk amewapongeza Makatibu wa UWT kwa kuhamasisha Wanachama kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili wa kadi za mfumo wa electric katika matawi yao.

 Ameyasema hayo huko Bububu mara baada ya kukabidhi kadi mpya kwa Makatibu wa Majimbo, Jimbo na matawi yaliomo katika Wilaya ya Mfenesini Kichama.

Amesema Wanachama wengi wamejitokeza kujisajili katika mfumo huo kutokana na  kuhamasishaji wa Viongozi hao  katika maeneo yao.

Hivyo amewaomba Viongozi hao kuendeleza juhudi zaidi hadi kufikia mwaka 2025 na kuendelea kukiweka Madarakani Chama Cha Mapinduzi.

"Wanawake tumehamasika, Takwimu ni kubwa tunaona misusruru ya Watu na sisi ni wengi mno, tusibweteke tuongeze juhudi, sote tunajuwa mtaji wa Chama cha siasa ni Wanachama, jamani ninawasihi kasi hii iendelee mpaka tuwaweke Vizongozi wetu Madarakani 2025" amesema Mbunge huyo.

Aidha amekiri kuzifahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili Makatibu hao na kuahidi kukaa na Viongozi wenzake kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi kichama Fatma Ali Ameir amesema idadi ya Wanachama wanaohitaji kadi ni kubwa hivyo ameomba kuongeza nyengine hali itakaporuhusu.

Hata hivyo amewaomba kubuni mikakati mbalimbali ya kuweza kuwaletea tija kwa maslahi ya CCM na Jumuiya zake.

Nao Makatibu hao  wamesema Kadi hizo zitawasaidia kuingiza Wanachama wapya na kuweza kusajiliwa kwa mfumo wa electronic na baadae kusajiliwa katika Daftari la kudumu la wapiga kura.

Mbali na hayo wameahidi kuyafànyia kázi maagizo waliopewa na Viongozi wao ili kuhakikisha wanaendelea kukibakisha madarakani Chama cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.