Habari za Punde

WAZIRI BYABATO AIPONGEZA BURUNDI KWA KUDUMISHA AMANI NA USALA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Leontine Nzeyimana katika picha ya pamoja alipowasili kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akihutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam
 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato amepoingeza Jamhuri ya Burundi kwa kuendelea kulinda na kudumisha amani na usalama nchini humo.

Naibu Waziri Byabato amasema hayo alipokuwa akihutubia Jumuiya ya Wadiplomasia na wageni wengine waalikwa kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Vilevile alibainisha kuwa katika kipindi hicho cha miaka 62 dunia imeshuhudi Taifa hilo likipiga hatua muhimu ya maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa na uchumi.

Hakika mtakubaliana nami kuwa katika kipindi cha miaka 

62, Burundi imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika nyanja 

za kisiasa na kiuchumi. Mathalani, kisiasa tangu kusainiwa 

kwa Mkataba wa Amani hapa jijini Dar es Salaam mwaka 

2006, Burundi imeweza kudumisha amani na usalama 

nchini kote pamoja na kukuza demokrasia na utawala 

bora” Alieleza Naibu Waziri Byabato

 

Mbali na hayo Waziri Byabato aliongeza kuwa Tanzania na 


Burundi zimeendelea kuwa na ushirikiano wa karibu wakati 


wote, ukichagizwa na mkaba uliosaniwa mwaka 1975 wa 


uanzishaji wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ambao ulifungua 


ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo 


elimu, afya, kilimo, biashara na uwekezaji, utalii,nishati, 


usafirishaji, ulinzi na usalama na masuala ya uhamiaji. 

 

Kwa upande wake Balozi wa Burundi nchini Tanzania 


Mhe. Leontine Nzeyimana alieleza kuwa katika kipindi cha 


miaka 62 ya uhuru, Taifa hilo linajivunia kuendelea 


kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Mataifa 


mbalimbali duniani na nchi jirani katika Kanda ya Afrika 


Mashariki.

 

Balozi Nzeyimana aliendelea kubainisha kuwa katika nyanja 


ya uchumi Burundi inaendelea kushirikiana na wadau 


mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Tanzania, ambapo mradi 


wa SGR unatarajiwa kuliunganisha Taifa hilo na Bandari ya 


Dar es Salaam hivyo kutoa mchango mkubwa katika 


kurahishisha na kuongeza biashara na uwekezaji kati ya 


Tanzania na Burundi.  

 

Takwimu zinaonyesha kuwa biashara kati ya Tanzania na 

Burundi inaendelea kukua ambapo ilifikia dola milioni 212.8 

mwaka 2022/2023 kutoka dola 61.3 milioni mwaka 

2017/2018. Huku takriban asilimia 95 ya mizigo ya Burundi 

ikipitia Bandari ya Dar es Salaam. 

 

Tanzania na Burundi zinashirikiana kwa karibu katika ngazi za 

kikanda na kimataifa ikiwemo EAC, ICGRL, AU, UN, Jumuiya 

ya Nchi zisizofungamana na Siasa za Upande wowote (NAM). 
 
Aidha Naibu Waziri Byabato alisisitiza dhamira ya Serikali ya 

Tanzania ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya 

Burundi ili kuimarisha zaidi uhusiano kwa manufaa ya pande 

zote mbili na  watu wake. Vile vile, kuendelea kuwa mshirika 

wa wakati wote na wa kuaminika wa Burundi kwenye masuala 

ya kikanda na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.