Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Mgeni Rasmin Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) Tumbatu Jongowe Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 1-10-2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wazee wa Jongowe Wilaya Ndogo ya Tumbatu, alipowasili katika bandari ya kijiji hicho kwa ajili ya kuhudhuria Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 1-10-2024.
WANANCHI wa Jongowe Wilaya Ndogo ya Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa ajili ya kuhudhuria Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 12-10-2024 katika Kijiji hicho

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuyafungua Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika katika Kijiji cha Jongowe Wilaya Ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja 1-10-2024, na (kushoto kwa Rais) Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe. Haji Omar Kheri na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Alhajj Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuyafungua Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) ya Kijiji cha Jongowe Tumbatu yaliyofanyika leo 1-10-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu iliyotolewa na Wananchi wa Jongowe Tumbatu, akikabidhiwa na Mwanafunzi wa Madrasatul Jawhar Atfal Jongowe Khamis Mohammed Hamza, wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 1-10-2024 katika Kijiji hicho

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Madrasatul Jawhar Atfal (kushoto kwa Rais) Khamis Mohammed Hamza na (kulia kwa Rais) Yahya Suleiman Haji, akiwa na zawadi maalumu aliyokabidhiwa wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(SAW) ya Kijiji cha Jongowe Tumbatu yaliyofanyika leo 1-10-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Jongowe Tumbatu wakati wa hafla ya Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 1-10-2024,katika Kijiji hicho cha Jongwe Wilaya Ndogo ya Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja

WANANCHI wa Kijiji cha Jongowe Tumbatu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Jongowe, wakati wa hafla ya Maulidi ya kuzawa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 12-10-2024 katika Kijiji hicho
WANANCHI wa Kijiji cha Jongowe Tumbatu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Jongowe, wakati wa hafla ya Maulidi ya kuzawa kwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika leo 12-10-2024 katika Kijiji hicho


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.