Afisa Uhusiano muandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Mbarak Hassan Haji Akitoa taarifa ya kupungua kwa mafuta kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa ZURA uliopo Maisara Mjini Unguja.
Na.Idara ya Habari (MAELEZO) Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Disemba 2024 ambapo bei hizo zimetajwa kupungua.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Afisa Uhusiano muandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Mbarak Hassan Haji katika ukumbi wa ZURA uliopo Maisara Mjini Unguja alisem bei hizo zitaanza kutumika kesho tarehe 09/12/2024.
Amesema bei ya Petrol imeshuka kutoka 2,882 Mwezi Novemba hadi kufikia 2,775 mwezi Disemba.
aidha alibainisha kuwa bei ya Dizel imeshuka kutoka 3,033 mwezi Novemba na kuuzwa 2,892 Kwa mwezi wa Disemba, huku mafuta ya ndege yakishuka kutoka 2,538 Novemba hadi kufikia shilingi 2,414 Disemba.
kuhusu mafuta ya taa Ofisa huyo amesema kuwa yatabaki kuuzwa Kwa bei ileile ya 3200 kwa mwezi Disemba kama ilivyouzwa Kwa mwezi Novemba.
Mwanzoni alieleza kuwa ZURA inapanga bei hizo kwa kuzingatia Wastani wa mwenendo wa Mabadiliko ya bei za mafuta Duniani, Gharama za uingizaji katika Bandari ya Dar-es-salaam na Tanga, gharama za mabadiliko ya fedha za kigeni zinazotumika kununulia mafuta, Gharama za Usafiri, Kodi za Tozo za Serikali na Kiwango cha faida kwa wauzaji wa Jumla na Reja Reja.
Hata hivyo asema kuwa bei za mafuta kwa mwezi Disemba, 2024 zimepungua kutokana na kupungua kwa wastani wa bei za mafuta katika soko la dunia, kupungua kwa gharama za uagizaji wa bidhaa za mafuta katika soko la dunia hadi kufika Zanzibar, pamoja na mabadiliko ya fedha za kigeni kwa shilingi ya Tanzania.
Mbali na hayo aliwakumbusha Wananchi kununua Mafuta katika Vituo halali vya kuuzia Mafuta na kudai Risiti za Kielectroniki kwani mbali na kutunza mapato lakini pia zitawasaidia wakati itakapotokea changamoto yoyote.
MAELEZO PICHA.
Afisa Uhusiano muandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Mbarak Hassan Haji Akitoa taarifa ya kupungua kwa mafuta kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa ZURA uliopo Maisara Mjini Unguja.
No comments:
Post a Comment