Habari za Punde

Madereva na Abiria Wapata Elimu ya Safiri Salama Majengo -Tunduma

Polisi Kata ya Majengo Wilaya ya Momba Mkoani Songwe Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mackyad Costantino Myumvi Disemba 16, 2024 ametoa elimu ya safiri salama kwa watumiaji wa vyombo vya moto na abiria katika stendi ya Zamani ya Tunduma.

Mkaguzi Myumvi akizungumza na madereva na abiria hao juu ya mradi wa safiri salama, ambapo aliwaeleza pindi wanapofanya safari wanatakiwa kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na abiria kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kwa madereva wazembe ili kuepusha ajali.

Aidha Mkaguzi Myumvi aliwataka madereva hao kuacha tabia ya kujihusisha kwenye vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kusafirisha wahalifu, mali za magendo pamoja na dawa za kulevya kama mirungi na bangi.

Pamoja na mambo mengine alihitimisha kwa kuwakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha ndani ya Mkoa wa Songwe kwa kuzingatia udereva wa kujihami ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.