Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Awasili Nchini Uganda Kumuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkutano wa Kilimo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2025 amewasili Kampala nchini Uganda ambako kesho atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu  Hassan katika Mkutano  kuhusu Mpango wa Kilimo  Afrika  utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya  Speke Resort and Conference Centre Munyonyo. Pichani,  Waziri Mkuu akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa  (kushoto) alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. wa pili kushoto ni Balozi wa Uganda nchini, Kanali Mstaafu , Fredy Mwesigy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Waziri wa Nchi anayeshugulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi  wa Uganda,  Fredrick Bwino  Kyakulaga (wa pili kushoto) alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda Januari 10, 2025 ambako  atamwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu  Hassan katika Mkutano  kuhusu Mpango wa Kilimo  Afrika  utakaofanyika  kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort anda Conference Centre Munyonyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi,   Fredrick Bwino Kyakulaga alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda ambako atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu  Hassan katika Mkutano  kuhusu Mpango wa Kilimo  Afrika  utakaofanyika  kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort and Conference Centre Munyonyo Januari 11, 2025. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa na kulia ni Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Mstaafu Fredy Mwesigye.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.