Khadija Khamis -WHVUM.
Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Muungano wa Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar( ZNCDs) Dr. .Said Gharib Bilali amewataka wasanii na waandishi wa habari kutumia mbinu mkakati ya utoaji elimu kwa jamii juu ya athari na ongezeko la maradhi yasioambukiza nchini.
Ameyasema hayo katika ukumbi wa Malaria, Mwanakwerekwe wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasanii na waandishi wa habari kuhusiana na ongezeko la maradhi yasioambukiza .
amesema waandishi wa habari walimu pamoja na wasanii iko haja ya kufikisha ujumbe kwa jamii ili kusaidia uelewa wa hali halisi ya maradhi na athari zake na jinsi ya kujikinga ili kuchukuwa tahadhali.
amesema maradhi hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kusababisha vifo vya watu wengi bila ya jamii kuwa na hofu ya maradhi hayo.
Aidha amesema maradhi hayo huathiri kiafya , kiuchumi na kifamilia,sababu zake hazieleweki moja kwa moja kwa kuwa na vichocheo vingi, hayapoi moja kwa moja na husababisha ulemavu wa kudumu
"Familia nyingi huyumba kutokana na baba au mama kupata maradhi hayo ambayo hutumia pesa nyingi katika matibabu jambo ambalo huengeza umasikini."alisema Dr Said.
amefahamisha watu wengi huchelewa kugundulika mapema kwa maradhi hayo kwa kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao.
"unapopata maradhi yasioambukiza utaendelea nayo hadi mwisho wa maisha yako ni vyema kuchukuwa tahadhari ya matumizi mabaya yanayochangia vichocheo vya maradhi hayo."amesema Dr Said.
Nae Katibu wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Maradhi ya Kisukari Omar Abdalla Ali akitoa mafunzo kwa wasanii amesema katika maradhi kumi yaliyoongoza Zanzibar maradhi sita ni Maradhi yasioambukiza .
ameeleza kuwa maradhi ya Presha na kupooza Viungo ( stroke) yameongoza kwa kulazwa wagonjwa, Kisukari, Saratani ya Matiti ,Saratani Ya Tenzi Dume,Saratani ya Mlango wa Kizazi, Koo, pamoja na utumbo wa haja kubwa .
ameeleza kwamba maradhi hayo husababishwa na vichocheo vingi ikiwemo matumizi ya pombe sigara,Tumbaku, mfumo mbaya wa ulaji, uzito kupitiliza,umri pamoja na historia katika familia .
Kwa upande wa Meneja wa Jumuiya ya Muungano wa watu wanaoishi na maradhi yasioambukiza Zanzibar (NCDs) Haji Khamis Fundi amesema Jumuiya hiyo imeanzishwa July 1, 2012 ikiwa ni muunganiko wa jumuiya mbali mbali za maradhi yasioambukiza kwa lengo la kupaza sauti zao.
ameeleza kuwa Muungano huo hushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia watu wanaoishi na maradhi yasioambukiza kwa kutetea na kutoa elimu kwa jamii.
Jumuiya ya Muungano wa Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar ni kati ya Muungano wa nchi sita za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi pamoja na Zanzibar ambazo hubadilishana uzoefu ,kupanga mbinu na mikakati ili kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
Nao washiriki hao wameishukuru Jumuiya hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahidi kuitumia sanaa yao katika kufikisha ujumbe kwa jamii ili kuweza kubadilisha tabia .
Vilevile waliiomba Serikali kuingiza katika mitaala elimu ya maradhi yasioambukia kwa wanafunzi tokea elimu ya msingi hadi sekondari pamoja na wanasiasa na Serikali kuungana katika kutoa elimu kwa Jamii
mafunzo hayo ya siku moja yametayarishwa na
Jumuiya ya Muungano wa Watu wanaoishi na Maradhi yasioambukiza Zanzibar ikifadhiliwa na World Diabets Foundation (WDF) Kupitia East Africa NCD Alliance (EANCDA)
No comments:
Post a Comment