Habari za Punde

WAFANYAKAZI WA ZMUX WAMUAGA MFANYAKAZI MWENZAO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ZMUX Hassan Simba Hassan akimkabidhi Zawadi Mfanyakazi Mstaafu Hawa Ibrahim Saburi alietimiza Miaka yake ya Utumishi  Kisheria kutoka mwaka 1984 hadi 2025  katika hafla maalum ya kumuaga iliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Kurusha Maudhui (ZMUX) wametakiwa kuwa waaminifu na wadilifu katika kazi zao za kila siku ili kuona kampuni hiyo inapiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi Rashid Hamdu Makame katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo   wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyokuwa mtumishi wa kampuni hiyo Hawa Ibrahim Saburi amesema uadilifu na uaminifu hufanya mfanyakazi kuwa ni kigezo chema na mfano wa kuigwa katika utendaji kazi.

Amesema mtumishi hufanyakazi kiuadilifu kwa lengo la kutekeleza vyema majukumu yake kwa kutoa huduma bora ili kuinuka kimaendeleo na kuipatia taasisi katika uendeshaji wa huduma zake.

Ameeleza utumishi wa Bi. Hawa Ibrahimu Saburi alikuwa ni mtumishi mwema aliyetukuka katika utekelezaji wa majukumu yake siku zote alizingatia sheria taratibu za kikazi ili kuona sehemu anayofanyia inakwenda vizuri na kuwasisitiza wafanyakazi wa taasisi hiyo kuwa kigezo kwa mama huyo na kufanyakazi kwa ushirikiano na upendo.

Akitoa wasifu wa Mstaafu huyo Afisa Utumishi wa tasisi hiyo Farida Haji Ali amesema Bi Hawa alizaliwa 26/3/1965 Michezani Unguja na alianza elimu ya msingi skuli ya Darajani Mwaka 1972 na kumaliza elimu yake ya sekondari kidato cha nne katika Skuli ya Hamamni mwaka 1982.

Amesema mwaka 1984 Bi Hawa ameajiriwa rasmi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi katika nafasi ya uhudumu wa ndege na ndani ya kipindi hicho na baadae kuhamishwa katika Taasisi tofaui na kupitia kada mbalimbali katika utumishi wake.

Ameeleza kuwa Bi Hawa amefanyakazi katika Idara ya Upigaji Chapa, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Idara ya Tamasha, Mila na Sanaa  na amepitia kada ya kuwa karani Kalamazuu, karani fedha, mshika fedha.

Afisa huyo amefahamisha kuwa Bi Hawa alihamishiwa katika Kampuni ya Urushaji Maudhui (ZMUX) Mwaka 2012 akiwa ni mchapakazi mahiri katika utendaji hadi  sasa kumalizia utumishi wake Serikalini.

Nae Mstaafu huyo Bi. Hawa Ibrahimu akitoa shukurani zake aliwaasa wafanyakazi kufanyakazi kwa ushirikiano na kupendana ili kufanikisha jukumu waliopewa pamoja na kuwataka kuwa waaminifu na wabunifu siku zote na kusaidiana pale mmoja wao anapohitajia  msaada. 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Raslimali watu katika kampuni ya kurusha Maudhui(ZMUX)Kahadija Ali Hassan akitoa taarifa fupi ya kumuaga aliekua Mfanyakazi wa Kampuni hio Hawa Ibrahim Saburi alietimiza miaka yake ya Utumishi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Kurusha Maudhui (ZMUX)Yussuf Haji Juma akitoa nasaha kwa Wafanyakazi katika  hafla ya kumuaga aliekua Mfanyakazi wa Kampuni hio Hawa Ibrahim Saburi alitimiza Miaka yake ya Utumishi kutoka mwaka 1984 hadi 2025   hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Aliekua Mfanyakazi wa Kampuni ya Kurusha Maudhui(ZMUX) Hawa Ibrahim Saburi akizungumza neno la Shukrani katika hafla ya Kumuaga ilioandaliwa na Kampuni hio baada ya kutimiza Miaka yake ya Utumishi kutoka mwaka 1984 hadi 2025  hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Rashid Hamdu Makame akitoa hotuba katika hafla ya kumuaga aliekua Mfanyakazi wa Kampuni ya Urushaji wa Maudhui (ZMUX)Hawa Ibrahim Saburi alietimiza Miaka yake ya Utumishi  Kisheria kutoka mwaka 1984 hadi 2025 hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Kurusha Maudhui (ZMUX)waliohudhuria katika hafla ya kumuaga aliekua Mfanyakazi wa Kampuni hio Hawa Ibrahim Saburi alitimiza Miaka yake ya Utumishi  Kisheria  kutoka mwaka 1984 hadi 2025    iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. 

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Kurusha Maudhui (ZMUX)Wakiwa katika Picha ya Pamoja katika hafla ya kumuaga aliekua Mfanyakazi wa Kampuni hio Hawa Ibrahim Saburi alitimiza Miaka yake ya Utumishi  Kisheria  kutoka mwaka 1984 hadi 2025  hafla   iliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Habari Maelezo Zanzibar .25/03/2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.