Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji Igunga

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji Safi ya Ziwa Victoria kutoka Mkomero hadi  Mgongoro katika kijiji cha Mwamayoka wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, Machi 12, 2025.  Wa pili kushoto ni  Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kushoto ni mbunge wa Igunga, Nicholaus Ngassa na kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,  Nassoro Hamdani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishika maji safi ya bomba wakati alipoweka jiwe la msingi la  ujenzi wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji Safi ya Ziwa Victoria kutoka mkomero hadi  Mgongoro, Machi 12, 2025.  Kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Maji Safi ya Ziwa Victoria kutoka mkomero hadi  Mgongoro, Machi 12, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.