Habari za Punde

Ilala Yapima Viwanja 66,029 Tayari Kumilikishwa kwa Wananchi

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam inaendesha zoezi la Kliniki ya Ardhi inayowasaidia wananchi wa Ilala kupata Hatimiliki za maeneo wanayomiliki ili kuwa na milki salama ya ardhi zao.

Akizungumzia zoezi hilo Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Rehema Mwinuka amesema viwanja vyote vinavyohusika katika zoezi la ukwamuaji wa urasimishaji katika jiji la Dar es salaam ni 66,029 tayari vimepimwa vinatarajiwa vitamilikishwa kwa wananchi ili wazitumie kama dhamana katika taasisi za fedha kujikwamua kiuchumi na kupunguza migogoro ya ardhi.

 

Bi. Rehema ametoa wito kwa wananchi wa Ilala jijini Dar es salaam kufika katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kivule ili wapate Hatimiliki za maeneo yao pamoja na kupata huduma nyingine za sekta ya ardhi ikiwemo kulipa kodi ya pango la ardhi za viwanja vyao.

 

Kliniki hiyo inahusisha wananchi kutoka maeneo ya Bombambili, Kerezange, Kivule, Magole 'A', Kitonga, Mbondole, Lubakaya, Pugu Kichangani, Pugu Station, Kitinye, Kitunda Relini, Kitunda Machimbo, Kipera, Kiyombo, Mogo, Sabasaba, Uwanja wa Ndege, Khanga, Kinyerezi, Bonyokwa na Amani–Liwiti.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.