Habari za Punde

SERIKALI YALIPA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 999 KWA WANANCHI 103 WA DODOMA KWA MIRADI YA MAJI

 

Afisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Ambrosi Siril akimsaidia mzee Peter Mazengo kusaini katika daftari la fidia katika eneo la Zuzu Nala jijini Dodoma ambao maeneo yao yamechukuliwa na DUWASA.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia 

Wizara ya Maji, imekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia yenye 

jumla ya Shilingi Milioni 999 kwa wananchi 103 ambao ardhi 

yao ilitwaliwa katika maeneo ya Nzuguni, Zuzu Nala, Nala 

Chihoni na Kibaigwa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa 

miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na 


Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Ulipaji wa fidia hizo, umeongozwa na Wizara ya Maji kwa 

kushirikiana na DUWASA, Wizara ya Ardhi na Viongozi wa 

Serikali za Mitaa wa maeneo husika, ambapo kwa eneo la 

Nzuguni, Wananchi 24 wamelipwa fidia ya Shilingi 

Milioni 148 tarehe 07 Agosti, 2025, Zuzu Nala Wananchi 51 

ambao wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 594  Agosti 11, 

2025, Nala Chihoni Wananchi 7 ambao walilipwa fidia yao ya 

Shilingi Milioni 58 tangu mwezi Aprili, 2025 na Kanda ya 

Kibaigwa Wananchi 23 wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 197 
na kukamilisha zoezi hilo Agosti 12, 2025.


Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph 

ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa kiasi hicho 

cha fedha kwa wananchi waliyotoa ardhi yao kupisha 

utekelezaji wa miradi ya maji.


"DUWASA, kwa niaba ya Wananchi wa maeneo ya Nzuguni, 

Zuzu Nala, Nala Chihoni na Kibaigwa, inaishukuru Serikali ya 

Awamu ya Sita na Wizara ya Maji kwa juhudi zao kubwa na 

ufanisi katika kuhakikisha ulipaji wa fidia kwa wakati kwa 

wananchi wetu," alisema Mhandisi Aron.


"Hatua hii ni muhimu sana kwa maeneo yaliyotekelezwa na 

yanayoendelea na utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati 

katika Jiji la Dodoma na Kanda ya Kibaigwa, hii inaonesha 

dhamira ya Serikali katika kulinda haki za wananchi wakati 

wa kutekeleza miradi ya maendeleo." Amesma Mhandisi Aron.


Kwa upande wa wakazi wa Kibaigwa, Bi. Josephina Paulo 

ameishukuru serikali kwa kuwasikiliza na kuwalipa fidia. 

Ameiomba serikali kwa kuwaona wanyonge na kuwafikia 

wengine ambao bado hawajalipwa wanasubiri kulipwa.


Naye Bwa.  Yohana Mwarabu ameshukuru serikali kwa 

kumjali na kumlipa kwani sasa ataenda kujenga nyumba 

nyingine ili aweze kuishi na familia yake kwani awali hakuwa 

na matumaini lakini kwa sasa anaamani.


Fidia hiyo ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa miradi 

mbalimbali ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia 

DUWASA iliyokusudiwa kuboresha upatikanaji wa majisafi na 

huduma za usafi wa mazingira ka wakazi wa jiji la Dodoma na 

maeneo mengine yanayohudumiwa na DUWASA.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.