Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe, Salama Mbarouk Khatib amesema Serikali inatoa fursa kwa Vijana ikiwemo za Kiuchumi Kijamii na Kiutamaduni hivyo ni vyema kwa Vijana kuzichangamkia fursa hizo.
Akiyasema hayo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Vijana ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya kuelekea Kilele cha Siku ya Vijana Kimataifa 2025. Katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Utaani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema wakati umefika kwa Vijana kujitambua Kwa kuchangamkia fursa zilizopo na kuunga mkono Jitihada za Serikali na Sekta Binafsi jambo ambalo litawasaidia Vijana kutatua changamoto zao ikiwemo ukosefu wa Ajira.
Pia amewataka Vijana hao kutambua kuwa Changamoto walizonazo kuzitumia kama fursa ya kuzikifikia ndoto zao na kuwa na mwamko wa kuzitengeneza fursa kupitia changamoto hizo.
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Kushirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa mema na mazuri wanayoendelea kuyafanya kwa kuwaletea Maendeleo endelevu kwa Wananchi wa Tanzania.
Amefahamisha kuwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanailinda Amani kabla na baada ya Uchaguzi.
"Nawaasa Vijana musikubali kwa namna yeyote ile kutumiwa na baadhi ya Wanasiasa kwa Maslahi yao na kuwa chanzo cha Uvunjifu wa Amani .
Aidha amezipongeza Idara ya Maendeleo ya Vijana na Baraza la Vijana Zanzibar Kwa kutatua changamoto na kuendeleza Ustawi wa Vijana kupitia maendeleo ya kiuchumi .
Nae Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau amewataka Vijana hao kuitumia Siku ya Vijana Kimataifa kwa kujitathmini na kuangalia mustakabali wao na mchango wao kwa Taifa na Maendeleo Endelevu.
Akielezea mada zitakazojadiliwa katika Kongamano hilo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Masoud Juma Haji amesema jumla ya mada tatu zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana katika ngazi za maamuzi, Vijana na Afya ya Akili na Vijana na fursa za Kiuchumi.
Kongamano hilo la siku moja limewashirikisha Vijana na Taasisi za Vijana kutoka Unguja na Pemba likibeba kauli mbiu ya Siku ya Vijana Kimataifa kwa mwaka 2025 " Wakati wangu ni Sasa, nitashiriki kuchagua na kuchaguliwa kwa Maendeleo Endelevu "
Imetolewa na Kitengo Cha Habari .
WHVUM.
No comments:
Post a Comment