Tanzania imeeleza kuziunga mkono nchi zinazoendelea zisizo na mlango wa bahari kutimiza matarajio na kukabiliana na changamoto zinazozikabili na kutoa wito wa kuchukua hatua za pamoja na kuufanya Mpango wa Awaza kubadilisha ahadi kuwa matokeo halisi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, ametoa kauli hiyo alipozungumza tarehe 6 Agosti
2025 kwenye Mkutano wa
Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nchi Zinazoendelea Zisizo na Bahari unaofanyika mjini Awaza, Turkmenistan.
Prof. Godius Kahyarara amesisitiza
juu ya umuhimu wa
kubadilisha Mpango wa Awaza kutoka kuwa tamko la Mkutano huo na kuufanya kuwa ramani ya kuelekea kwenya matokeo chanya ya
maendeleo jumuishi.
“Tanzania si nchi isiyo na bahari, lakini nafasi yetu ya kimkakati kama nchi
yenye Bahari na njia ya
usafiri inatufanya kuwa kitovu cha muunganiko wa kikanda katika ukanda wa Afrika Mashariki na
Kusini mwa Afrika.
Bandari zetu, njia za usafirishaji, na miundombinu ya usafirishaji hutumika
kama mishipa muhimu kwa uchumi wa nchi kadhaa zisizo na mlango wa bahari, ikiwemo Zambia,
Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” alieleza
Prof. Kahyarara.
Alihimiza kuwa
Tanzania itaendelea kujitolea kutoa suluhisho bora, salama na linalostahimili
mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya kurahisisha biashara na maendeleo kwa
majirani zake wasio na mlango wa bahari.
“Tunaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya uwekezaji kupitia Ukanda wa Kati
na TAZARA, kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, kupanua miundombinu ya reli na
barabara, pamoja na kurahisisha taratibu za forodha mipakani kwa mujibu wa
Mkataba wa WTO wa Kurahisisha
Biashara na soko la eneo huru
la Afrika (AfCFTA).
Tunaamini kuwa kubadilisha njia za usafirishaji kuwa kanda za kiuchumi ni hatua
muhimu kwa mageuzi ya kiuchumi, ushirikiano wa kikanda, na ustawi wa pamoja,”
alisisitiza.
Alieleza kuwa Tanzania imedhamiria kuendelea kushirikiana kwa njia za uwili, ushirikiano wa Kusini
kwa Kusini, ushirikiano wa pembe tatu na majukwaa ya kikanda ili kusaidia nchi
zisizo na mlango wa bahari
kuvuka vizingiti vya kimfumo na kuwa nchi zenye uhusiano wa moja kwa moja na
masoko.
Prof. Kahyarara alisema Tanzania inasisitiza haja ya kuchukua hatua za
pamoja ili kuhakikisha Mpango wa Awaza unakuwa siyo tu tamko la nia, bali ni
ramani ya kweli ya mageuzi.
“Mkutano huu uwe chombo cha mabadiliko ambacho kitaashiria mwanzo mpya—ambapo
maendeleo ya nchi yoyote hayatekwi
na jiografia yake, bali mshikamano na maendeleo ya pamoja ndiyo yanayoongoza
safari yetu ya pamoja kuelekea 2030 na baada ya hapo,” alisisitiza.
Alisisitiza kuwa Mpango wa Awaza haupaswi kubaki kama hati isiyotenda kazi,
bali uwe ramani hai ya mageuzi inayoungwa mkono kwa vitendo na washirika wa
maendeleo, taasisi za kifedha, na nchi jirani za pwani kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment