Wito huo umetolewa na Mratibu wa Kitengo cha Uhamasishaji na Mabadiliko ya Tabia, Programu Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya Zanzibar bi Munaa Yussuf Mohamed wakati alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Mikunguni Wilaya ya Mjini.
Amesema makundi hataraishi, yanaweza kupelekea kupata maambukizi ya Ukimwi, Homa ya ini B na C, Maradhi ya kujamiiana pamoja na Ngozi.
Aidha amewataka Wananchi kubadilika kwa kuhamasisha Vijana kupima Afya zao ili kujikinga na Changamoto ya kupata maradhi ya Afya ya Akili.
Hata hivyo amesema Serikali, inaimarisha maendeleo kupitia sekta mbali mbali ikiwemo Elimu, Efya, Miundombinu ya jamii ili kuwawezesha Vijana kupata maendeleo.
Kwa upande wake Daudi Kassim kutoka Taasisi ya Pamoja Youth Initiative amewataka Vijana wasikubali kutumiwa vibaya na Watu wasiopenda maendeleo kwa kujishirikisha katika kufanya vurugu.
Aidha amesema Vijana ni nguvu kazi na tegemeo la Taifa hivyo ni muhimu kuwa Wazalendo wa kuijenga Nchi yao kwa maslahi yao na Taifa kwa Ujumla.
Nao baadhi ya Vijana waliopatiwa elimu hiyo wamesema, imewapa mwanga na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo waliopewa ikiwemo kujikinga na Vishawishi vinavyoweza kuwaharibia kustakbali nzuri wa maisha yao ya sasa na baadae.
Kongamano hilo la Vijana, ikiwa ni miongoni mwa shamrashara za kuelekea maadhimisho ya wiki ya Vijana, limeandaliwa na Taasisi ya Youth Friends Service, Pamoja Youth Iniativu, Zanzibar Intergrated HIV Hepaties TB,Lepresy Programme kwa kushirikiana na Kituo Rafiki kwa Vijana mahonda, Rahaleo na KMKM.
Maadhimisho ya siku ya Vijana kitaifa 2025, yanatarajiwa kufanyika Skuli ya Utaani Kisiwani Pemba, Ogasti, 12, 2025 na kauli mbiyu ni “Wakati wangu ni sasa nitashiriki kuchagua na kuchaguliwa kwa Maendeleo Endelevu” ambapo jumla ya Vijana 240 wameshiriki katika Kongamano hilo.
Imetolewa na kitengo cha Habari,
WHVUM.
No comments:
Post a Comment