Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Ndugu Fatma Hamad Rajab amezitaka Taasisi na Wadau mbali mbali wa Maendeleo ya Vijana kutoa Mafunzo ya muongozo wa Stadi za Maisha kwa Vijana ili kuweza kujitambua .
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Muongozo wa Kitaifa wa Stadi za Maisha Kwa Vijana walio nje ya Skuli Zanzibar Katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul - Wakil Kikwajuni.
Amesema Vijana wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali katika jamii pamoja na familia, jambo ambalo husababisha msongo wa mawazo na hupelekea kujiingiza Katika Tabia hatarishi.
Aidha amesema muongozo huo unalenga kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo Afya ya Uzazi, unyanyasaji wa kijinsia, madawa ya Kulevya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano lishe na Ajira Kwa vijana.
Amefahamisha kuwa Stadi hizi huwafundisha Vijana namna ya kujiamini, Kudhibiti hisia, kutatua changamoto pamoja na kufanya Maamuzi sahihi.
"Suala la Stadi za Maisha ni ujuzi na fani muhimu za kuwawezesha Vijana kukabiliana na changamoto za Kila siku Kwa kuweza kufanya Maamuzi sahihi na kuishi Kwa Amani na Furaha na watu wengine " amesema Katibu Fatma
Amesema Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Wadau mbali mbali wa Maendeleo walifanya mchakato wa marekebisho ya Mwaka 2019 ili kukidhi mahitaji ya Sasa.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Shaib ibarahim Mohamed amesema lengo la muongozo wa Stadi za Maisha Kwa Vijana ambao wapo nje ya Skuli ni kuzitaka Taasisi na Asasi za Kiraia kutoa Mafunzo sahihi yanayoendana na mazingira, Utamaduni wa Zanzibar pamoja na Sheria za nchi.
Nae Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia Watoto UNICEF Laxmi Bhawan amesema kitini hicho kitakuwa ni chachu ya kuleta matokeo chanya Katika Maisha ya vizazi vya Sasa na vijavyo..
Amesema Mafunzo ya Stadi za maisha yatasaidia kumbadilisha Kijana kiakili, kihisia, kiimani pamoja na kimuonekano jambo ambalo husaidia kuondokana na changamoto na kuwa na maamuzi sahihi.
No comments:
Post a Comment