Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya Vijana Zanzibar Shaibu Ibrahim Mohammed ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Stadi za maisha kwa Vijana waelimishaji Rika huko katika kituo cha Mafunzo ya Vijana Bweleo Wilaya ya Magharibi "B " Unguja.
Amesema Serikali kupitia Idara ya maendeleo ya Vijana imeandaa mafunzo hayo ili kuwewezesha Vijana kukabiliana na Changamoto zilizopo, kupata uelewa sambamba na kutoa mchango kwa Taifa.
Aidha amesema Serikali ina jukumu la kupanga na kuratibu masuala ya Vijana ikiwemo kuandaa Sera, Mikakati na Mipango ili kuwashirikisha Vijana na kuwanyanyua kiuchumi.
Mapema akitoa maelezo katika Mafunzo hayo, Mratibu Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar Salma Kombo Mohammed amewataka Vijana hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili kuweza kufikia malengo yaliopangwa na Serikali kupitia Idara hiyo.
Hata hivyo, amesema Vijana hao ambao ni wawili (2) kutoka kila Shehia, kila mmoja anawajibu wa kuwafikia kiasi ya Vijana 60 kwa mwaka.
Jumla ya Vijana 100 kutoka Wilaya za Unguja, wameshiriki katika Mafunzo hayo ya siku (5) ambayo yameandaliwa na Idara ya maendeleo ya Vijana chini ya Ufadhili wa Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF).
Imetolewa na Kitengo Cha Habari, WHVUM.
No comments:
Post a Comment