Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amewataka Wananchi Kuendeleza Amani kwa Maendeleo ya Nchi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kwa ajili ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 7-11-2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Waumini wa Dini ya Kiislamu, baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 7-11-2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza wananchi kuendeleza utaratibu wa kuiombea nchi amani ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unafanikiwa kwa ufanisi.

Akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa, Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 7 Novemba 2025.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema  baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu kwa amani, ni muhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendelea kumuomba ili amani hiyo idumu.

Halikadhalika, Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kazi nzuri iliyofanyika kuombea amani wakati wa uchaguzi inapaswa kuendelezwa kwa juhudi kubwa zaidi.

Rais Mwinyi amesisitiza kuwa ni neema kubwa kwa Zanzibar kubaki na umoja, amani, utulivu, na mshikamano baada ya uchaguzi, na kuwataka viongozi wa dini na waumini kuendelea kuiombea nchi ili ibaki salama na yenye maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Viongozi mbalimbali na Wananchi baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 7-11-2025.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.