NAIROBI, Kenya
VIKOSI vya usalama nchini Kenya, vimesema viko katika mkondo wa lala salama katika kudhibiti jengo zima la Westgate. Serikali imesema mateka wote wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia jana.
Taarifa hizo zinasema mmoja ya alieuawa ni mwanamke wa kizungu raia wa Uingereza, hali inayothibitisha kwamba Samantha Lewthwaite, maarufu ‘White Widow’ (mjane mweupe) alikuwa miongoni mwa magaidi.
Siku ya Jumamosi mmoja ya maafisa wa usalama alisema alimuona mwanamke wa kizungu akitoa maelekezo kwa washambuliaji kwa lugha ya kiarabu.
Magaidi hao waliuawa katika operesheni ya kuwakomboa mateka waliokuwa wakiwashikilia.
Aidha jeshi la ulinzi la Kenya (KDF) kimethibitisha wanajeshi wake watatu wameuawa na wengine wanane wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu hospitali.
Serikali ya Uingereza imethibitisha miongoni mwa waliouawa wamo raia wake sita.
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa.
Duru kutoka Shirika la AFP zinasema majeshi ya Kenya bado yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.
Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na miripuko ilisikika mapema jana asubuhi kutoka katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.
1 Comments
Mungu awape moyo wa subira ndugu zetu wa kenya, sisi hapa znz, tume fanikwa, kuwazibiti, viongozi wa maharamia, sasa wanajita ugonjwa, ili wapate kutoka, waje wafanye uharibifu, ujanja wao umejulikana, wasahau, sisi tunataka tupumue, mungu hataki, dini yake, itiwe doa, na wahuni, sasa wambane na sheria, ingiwa tuna msiba ulowakuta nduzetu, wakenya, mmajiribio yao yote yamekwama kwa kuwa vingozi wa ubilis, wamehifaziwa, wanajaribu, kumwagia watu tindikali, kutisha, hatuwatoi waikabili sheria
ReplyDelete