Hekeheka golini kwa timu ya Kilimani City wakati wa mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Mjini mchezo uliofanyika uwanja wa Ziwani Bomani.
Mchezaji wa timu ya Kilimani City akiondoa mpira galini kwake na huku mchezaji wa timu ya Kijangwani akiwa karibu yake,
Mdau wa mchezo wa Soka Zanzibar Kiski akiwasili katika kiwanja cha
Bomani kuangalia mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Mjini kati ya Kilimani City
na Kijangwani, mchezo uliofanyika uwanja wa Bomanin Ziwani Polisi.
Mshambuliaji wa timu ya Kijangwani mwenye mpira akimpita beki wa timu ya Kilimani City, wakati wa mchezo wa Ligi ya Wilaya ya Mjinin Daraja la Pili.
Hekaheka golini kw timu ya Kilimani City golikipa wa timu hiyo akwa juu na mpira akiokoa hatari hiyo, wakati wa mchezo wa ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini mcheo uliofanyika uwanja wa Bomanin Ziwani.Polisi.
Kocha wa timu ya Kilimani City akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Kocha wa timu ya Kijangwani akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza wakati timu yake ikiwa imefungwa mabao 2--0.
1 Comments
mimi ni Rais wa KIlimani City Khamis Shaali nimefurahi kuona taarifa ya mechi yetu ya mwanzo kwa msimu wa 2013-2014, aidha napenda kukujulisha kuwa tumefungua blog yetu na tunapost habari mbali mbali za timu yetu, tafadhali tembelea blog yetu na tumekuruhusu kuzitumia taarifa zetu kwa kazi zako za zannews www.kilimanicityfc.blogspot.com, pia tuna afisa habari wetu da Zainab Haroub unaweza kuwasiliana nae kwa habari za timu yetu 0242231990 wakati wa saa za kazi.
ReplyDelete