ZOEZI LA KUIOPOA MV. FATIH BADO LAWAPA TAABU WATAALAM
Na Mwantanga Ame
MKURUGENZI Mkuu Shirika la Bandari Zanzibar, Mustafa Aboud Jumbe, ameeleza kwamba zoezi la uokoaji wa meli iliyozama ya MV. Fatih limekuwa gumu kutokana na kukosekana ramani ya meli hiyo pamoja na ushirikiano mdogo kutoka kwa mmiliki wa meli hiyo.
Mustafa aliyasema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Afisini kwake Bandarini Zanzibar.
Kauli ya Mkurugenzi huyo imekuja wakati zoezi la kuiopoa meli hiyo likiwa halijafanikiwa kwa zaidi ya siku ya sita sasa. Meli hiyo ilizama Mei 29, bandarini Zanzibar.
Alisema kazi ya uokoaji imekuwa ikibadilika kwa kuwepo matumaini halafu yakatoweka, kunatokana na kufanyakazi kwenye mazingira magumu ya kitaalamu kutokana na kukosekana ramani ya meli hiyo pamoja na ushirikiano mdogo kutoka kwa wamiliki wake.
Alisema vikosi vya uokozi na kamati ya maafa,kwa kushirikiana na shirika la Bandari na Mamlaka ya Bandari Tanzania wamefanya jitihada kubwa ya kuiopoa bila ya kuyafahamu maeneo muhimu ya kuishika meli hiyo.
Hata hivyo, alisema bado ipo tamaa ya kufanikiwa kwa vile mkazo umewekwa katika kuigeuza meli hiyo.
"Hatuna ushirikiano na wanaomiliki meli hii tunaambiwa Chifu injinia na Chifu Afisa hawapo wako juu ....lakini mpaka hii leo hawajajitokeza angalau wakatoa ramani ya chombo chao, kwani kama wana wasi wasi wa maisha yao basi wangeliweza kwenda Polisi na kutoa taarifa zao lakini wote hawaonekani", alisema Mkurugenzi huyo.
Alisema idadi waliokuwemo kwenye chombo hicho iliyotolewa na Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam ni ya abiria 25, mabaharia 13 na mzigo wa tani arobaini lakini bado kuna utata kutokana na kwamba watu walionusurika ni 33 huku waliokufa ni sita, hali inayohitaji kuthibitishwa na wamiliki hao.
Mkurugenzi huyo alisema vikwazo hivyo vimesababisha hali kuwa ngumu na kulitia hasara shirika na serikali.

"Tunakosa fedha nyingi sasa kama dola za Kimarekani 30,000, bidhaa nyingi hazitoki inabidi tuingize mtu mmoja mmoja kutoa bidhaa zake, huku kuna meli imeshafika na mizigo wenye mali zao wanataka kutoa na nyengine inakuja lakini tumesitisha kwa kazi hii" alisema Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo alisema pamoja na matatizo yote yaliojitokeza hadi sasa kazi ya uokoaji itaendelea ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana.
Kuhusu hitilafu zinazotokea kwa chombo cha Ndovu, Mustafa alisema inasababishwa na kuwa MV. Fatih kuwa na uzito wa zaidi ya tani 300 kiasi ambacho kimesababisha kuwa na kazi ya ziada katika kuivuta meli hiyo.
Aidha Mkurugenzi huyo pia alikataa madai ya kuhusishwa na tukio hilo kama alichangia kutokana na kutoiruhusu meli hiyo kuegesha eneo la Forodhani.
"Mimi nilikuwa nyumbani kwangu na nilipoambiwa tu nilikuja hapa baada ya dakika 15 shughuli za uokoaji zikaanza kufanyika kiasi ambacho mambo mengi tuliyafanya usiku huo sasa hapo lawama zinatokea wapi", alisema.
Nae Ofisa Mkuu wa meli hiyo Moris Kunambi, ambaye alijitokeza kwa mara ya kwanza, alisema meli hiyo haikuwa na matatizo wakati wakiwa njiani na wameshangaa kutokea tukio hilo wakiwa bandarini.
Alipoulizwa ni kwanini walishindwa kutoa ushirikiano na Shirika la Bandari alisema siku ya kwanza walifanya hivyo lakini kutokana na kuwapo kwa ulinzi katika bandari hiyo walizuiliwa na askari waliokuwa katika lango kuu kuingia ndani.
Alifahamisha baada ya kukataliwa kuingia ndani waliona haina haja ya kulazimisha na ndipo jana walipoamua kujitokeza tena wakiwa na ramani iliyochorwa kwa mkono na kumkabidhi Mkurugenzi wa Shirika la Bandari.
"Taarifa hizi sio za kweli na wala sizifahamu kwani kama tungelikuwa tumeona kuna hatari basi tulikuwa na uwezo wa kuwapa abiria wetu makoti ya kuokolea maisha sasa hakuna ukweli kwani tulifunga gati" alisema Kunambi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Bandari, Abdi Omar, alisema zoezi hilo litafanyika tena leo baada ya kuzuka matatizo ya kiufundi katika meli ya ndovu ambayo ilitakiwa kutumika katika uvutaji wa MV. Fatihi.
Hadi mchana wa jana ambapo zoezi hilo lilitarajiwa kufanyika majira ya saa 8.00 mchana baada ya maji kujaa lilishindikana tena baada ya kujitokeza kwa matatizo ya kiufundi katika tishari la
Ndovu ambalo lilitarajiwa kuifanya kazi hiyo kwa kutumia chombo hicho.
Meli ya Mv. Fatih ilizama mwishoni mwa wiki iliopita ambapo zaidi ya watu 33 walinusurika kufa na sita walifariki dunia na mali za mamilioni ya fedha kupotea.

No comments:
Post a Comment