Na Mwantanga Ame-- ZANZIBAR LEO
UOKOAJI MV. FATIH BANDARINI ZANZIBAR
KAZI za uokoaji wa Meli ya MV Fatih iliozama katika Bandari ya Zanzibar zimeingia siku ya sita jana huku kukiwa hakuna mafanikio ya kuiinua baada vyuma vilivyotegemewa kuinua meli hiyo kuchanika.
Uinuaji wa meli hiyo ulifanyika kuanzia saa 6:00 mchana jana, kwa kutumia Mv. Ndovu iliyokuwa ikisaidina na Chatu na ‘tag’ ya Shirika la Bandari .
Katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo lilishindikana kutokana na kujitokeza tatizo la kukatika nyororo wa chuma uliofungwa meli hiyo.
Hitilafu katika chombo ilitokea huku kukiwa kumeanza kuonesha matumaini ya kuinua meli hiyo na kutokeza juu kiasi na kuonekana ‘propela’ lakini ghafla myororo ulikatika na kurejea tena habarini.
Jaribio la awamu ya pili kuinua meli hiyo lililofanyika majira ya saa 10:13 jioni lakini pia halikufanikiwa baada ya dakika zaidi ya 10 kupita bila mafanikio baada ya kuchanika sehemu iliyofungwa mnyororo huo.
Hatua hiyo ilianza kutoa matumini ya mafanikio katika kazi hiyo nzito ilioanza Mei 30 lakini baadae yakatoweka.
Matumaini hayo yalikuja baada ya dakika 27 ambapo meli hiyo ilivutwa kiasi cha kuonekana sehemu za madirisha lakini nayo ilikwama baada ya kuchanika sehemu iliyofungwa na kutmbukia tena baharini.
Hata hivyo kazi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo katika wakati ambao kina cha maji kitakua kimeongezeka kusaidia kurahisisha kuinua meli hiyo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Bandari Abdi Omar,, alisema zoezi hilo limeshindwa kufanikiwa kwa kuwa kina cha maji kilikua ni kidogo jambo ambalo lilikwaza ufanisi wa kazi hiyo.
Alisema lengo la kuinua meli hiyo ni kuitoa katika upande wa kusini na kuipeleka Kaskazini lakini kutokana na maji ya bahari kuwa kidogo halikuweza kupata mafanikio.
Awali alisema mafundi wa shirika na waokoaji wanaangalia namna ya kufunga tena mnyororo huo kwenye eneo jengine ili kuiinua lakini nalo lilishindikana hapo jioni.
Alisema pia wanalifanyia kazi tatizo la baadhi ya vifaa vilivyopata hitilifu katika chombo kinachotumika kuivuta meli hiyo.
Mkurugenzi huyo alieleza matumaini yake kuwa baada ya jitihada hizo kuna uwezekano wa kupatikana mafanikio.
Hata hivyo alisema kwamba Shirika halijafikiria umuhimu wa kutafuta msaada kutoka nje wa kuokoa meli hiyo ambayo hadi sasa inafikiriwa kuna maidi waliokwama ndani ya meli hiyo.
Alisema kazi ya kuinua meli ni nzito zaidi na haifanani na ya uinuaji wa jahazi ambayo huchukua muda wa siku tano hadi saba na shirika hilo bado halijashindwa kuineua meli hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Mustafa Aboud Jumbe alisema shirika lake limekuwa likifanya kazi za aina hiyo kwa muda mrefu na imekuwa ikifahamu mazingira ya ugumu wa uokoaji.
Hali katika eneo la bandari iko katika utulivu kutokana na kuwapo kwa ulinzi wa vikosi vya Polisi na Jeshi la JWTZ, katika lango kuu la Bandari hiyo.
Meli ya Mv. Fatih ilizama Mei 29, katika Bandari ya Zanzibar, wakati ikitokea Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu sita na 33 walinusurika baada ya kuokolewa na wengine kuwahi kushuka katika meli hiyo.
Ndani ya meli hiyo inadaiwa na Nahodha wake alibeba abiria 25 na Mabaharia 13 na mzigo wa tani 40 ikiwemo gari mbili.
Tangu kuzama kwa meli hiyo tayari mali kadhaa zimeweza kupatikana zikiwemo baadhi ya vipande vya mbao, gari mmoja aina ya trela makopo ya rangi, sabuni, vipodozi, katuni za juisi na magodoro ambapo mali hizo zinakiisiwa kufika zaidi ya milioni 60 zimeokotwa na kuhifadhiwa katika eneo maalum.
Wakati mali hizo zikiwa ndizo zilizookolewa hali ya bahari eneo ambalo meli hiyo imebiruka kumeonekana kutanda bidhaa ya Maharagwe yaliokuwa yakielea, jambo ambalo lilisababisha kuwapo kwa harufu kali mchanganyiko ikiwemo ya hofu ya miili ya watu zaidi wanaodaiwa kuwamo katika meli hiyo.

No comments:
Post a Comment