Habari za Punde

ILE SIKU YA KINYAN'GANYIRO CHA KUCHUKUA FOMU YA URAIS KUPITIA CCM IMEWADIA

MHE. ALI JUMA SHAMHUNA.


Shamuhuna Asema Amefanya Kazi Tokea Awamu ya Kwanza


Atahakikisha Maslahi ya Zanzibar Yanalindwa


Ataridhia Mabadiliko Yanayolinda Muungano


NAIBU Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari Utamaduni na Mchezo, Ali Juma Shamuhuna
amesema yeye ni kiongozi shupavu wa kisiasa anayekubali mabadiliko ambayo hayageuzi misingi ya kisiasa.
Alisema kwa vile amefanya kazi na awamu zote sita nchini, ataridhia mabadiliko yatakayolinda Muungano, yatakayoheshimu misingi ya CCM katika utawala, uchumi na maendeleo.
Aidha alieleza kuwa mabadiliko mengine ni yake yanayotetea usawa wa binaadamu, jinsia na kuheshimu katiba, sheria na kanuni za kuendesha nchi katika utawala bora.
Alifafanua kuwa, endapo atapewa ridhaa ataendeleza sera zilizopo na kubuni sera na mipango mipya itakayosaidia kuendeleza uchumi wa Zanzibar na ustawi wa wananchi wake, kwa kuhakikisha maisha yao yanaimarika siku hadi siku.
Alisema atahakikisha mafuta yatabakia kuwa si ya Muungano ingawa katika katiba ni Muungano lakini kimantiki ni ya Zanzibar, hivyo ataendeleza mazungumzo katika kutatulia hilo ili yaweze kusaidia kukuza uchumi wa visiwa hivi.
Akizungumzia msimamo wake juu ya kura ya maoni, alisema anaheshimu maamuzi ya Butiama na Chama chake, lakini alishauri suala hilo waachiwe wananchi waweze kuamua.
Shamuhuna aliijinadi kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Zanzibar na anafaa lakini wananchi na wapiga kura ndiyo wenye uwezo, haki na uhuru wa kumpima, kumchambua na hatimaye kuamua kama anafaa.
NAIBU WAZIRI KIONGOZI NA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR ALI JUMA SHAMHUNA AKIOMBA DUWA KATIKA KABURI LA MAREHEMU MZEE KARUME KABLA YA KUCHUKUWA FOMU YA URAIS.
KATIBU KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR ITIKADI NA UENEZI VUAI ALI VUAI AKIMKABIDHI FOMU YA URAIS MHE. ALI JUMA SHAMHUNA. ALIPOFIKA KUCHUKUA FOMU.


WAANDISHI WAKIJIWEKA TAYARI KUPATA TUKIO LA KUCHUKUWA FOMU YA URAIS MMOJA WA MGOMBEA.
NAIBU WAZIRI KIONGOZI NA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ALI JUMA SHAMHUNA AKITOWA DHAMIRA YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA URAIS.

MUANDISHI WA REDIO ONE MAULID HAMADI AKIULIZA SUALI KWA MGOMBEA BAADA YA KUCHUKUA FOMU NA KUTOWA DHAMIRA YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VEIW MIGOMBANI.

MUANDISHI WA BBC ALI SALEH AKIULIZA SUALI KWA MGOMBEA NAFASI YA URAIS KUPITIA CCM.

MUANDISHI MUANDAMIZI JABIR IDRISA WA GAZETI LA MWANAHALISI AKIMUULIZA SUALI HE, SHAMHUNA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUCHUKUWA FOMU,

WAANDISHI WAKIWA KATIKA MKUTANO NA MMOJA WAGOMBEA KUTEULIWA NA CHAMA CHAKE KUGOMBEA NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR WAKIWA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VEIW MIGOMBANI.

WANANCHI WAKIMSIKILIZA NAIBU WAZIRI KIONGOZI NA WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR ALI JUMA SHAMHUNA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI BAADA YA KUCHUKUWA FOMU YA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA CCM.









MHE. SHAMSI VUAI NAHODHA.

Nitaendeleza umoja, amani, mshikamano wa Wazanzibari
Siasa za malumbano, chuki hazina nafasi
Atasimamia nidhamu, uwajibikaji serikalini

Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha jana aliungana na wagombea wengine sita wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi katia uchukuaji fomu za kuwania nafasi hiyo.
Alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati Maalum, Itikadi na Uenezi, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui.
Akizungumza na waandishi wa habari, alisema akichaguliwa atahakikisha amani, utulivu na umoja unaendelea kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya kiuchumi na kujenga Zanzibar yenye matumaini kwa wananchi wake.
Alieleza siasa za malumbano na za chuki hazina nafasi katika Zanzibar kwa sasa baada ya maridhiano yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ambapo aliahidi kuiendeleza hali hiyo.
Alifahamisha kuwa, Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika nyanja ya elimu ili kuwapatia taaluma iliyobora wananchi katika kukabiliana na soko la Afrika Mashariki na Kati, sambamba na kuimarisha kilimo hasa cha umwagiliaji na uvuvi .
Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Karume imefanya kazi vizuri katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Unguja na Pemba, katika kusambaza miuondo mbinu ya barabara, maji, afya na elimu, ambapo matunda hayo atayaendeleza.
Hata hivyo, alisema atakakikisha anasimamia uwajibikaji na nidhamu katika sehemu za kazi kuanzia kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi hadi kwa wananchi wa chini katika kufanya kazi kwa ufasini katika kuibadilisha Zanzibar.



WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA AKIKABIDHIWA FOMU YA URAIS NA KATIBU KAMATI MAALUM YA NEC ITIKADI NA UENEZI VUAI ALI VUAI (KULIA)AFISI KUU YA CCM KISUWANDUI.
WAANDISHI WAKIWA KAZINI KILA MTU AKITAKA PICHA BORA KWA WATAZAMAJI WAKE NA WASOMAJI
WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA TANZANIA DHAMIRA YAKE YA KUCHUKUWA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA BWAWANI BAADA YA KUCHUKUA FOMU HIYO.

WANANCHI NA WANACHAMA WA CCM WAKIMSIKILIZA WAZIRI KIONGOZI SHAMSI VUAI NAHODHA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA BWAWANI DHAMIRA YAKE YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM.
WANACHAMA WA CCM WAKIMSIKILIZA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUTEULIWA NA CHAMA CHAKE KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR, AKIWA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA BWAWANI.
WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKILIZA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.