Habari za Punde

ZAMU YA DK MOHAMMED GHARIB BILAL ILIVYOKUWA




Bilal Aahidi Kuleta Maridhiano Kwa Wazanzibari

Asema Atasimamia Rasilimali Za Nchi

Aahidi Kuimarisha Elimu, Afya, Ajira Kwa Wote

WAZIRI Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema iwapo jina lake litapitishwa na baadae kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, atahakikisha analeta maridhiano ya Wazanzibari wote.
Dk. Bilal alitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View jana, baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti hicho katika uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi wa Oktoba.
Alisema jambo lililofanywa na Rais Amani Abeid Karume anayemaliza muda wake na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad kufungua ukurasa mpya wa maelewano ni jema lakini linapaswa kwenda mbali zaidi ili kujenga umoja na maridhiano kwa wananchi wote wa visiwa hivi.
Alisema katika dunia hakuna mtu asiyependa maelewano, na kwamba kama atachaguliwa serikali yake haitakuwa na siasa za kulipa kisasi kwa kuwa yeye binafsi haoni kama amekosewa na yeyote.
Akizungumzia namna atakavyoleta ustawi wa kiuchumi kwa Zanzibar na wananchi wake, Dk. Bilal alisema atahakikisha rasilimali zote zilizomo nchini zinatumiwa kwa manufaa ya Wazanzibari wote.
Alisisitiza kuwa hatakuwa na muhali kwa yeyote katika suala la kuwajibika, na kuweka wazi kuwa kila atayepewa dhamana atalazimika kuitimiza mujibu wake.
Waziri Kiongozi huyo Mstaafu, alieleza kuwa pamoja na maendeleo yaliyofikiwa katika sekta za elimu na afya, ni lazima ziimarishwe.
MGOBEA AKIWA NA WAPAMBE WEAKE WAKISOMA DUWA KATIKA KABURI LA MAREHEMU MZEE ABEID KARUME KABLA YA KUCHUKUWA FOMU.

WANACHAMA WA CCM WAKISUHUDIA UTOAJI WA FOMU YA URAIS KATIKA AFISI KUU YA CHAMA KISUWADUI.


KATIBU KAMATI MAALUM YA NEC ZANZIBAR ITIKADI NA UENEZI YA CCM ZANZIBAR VUAI. ALI VUAI, AKIMKABIDHI FOMU YA KUGOMBEA URAIS MGE DK. MOHAMMED GHARIB BILAL AFISI KUU YA CCM KISUWANDUI.



WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU MHE. MOHAMMED GHARIB BILAL AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI BAADA YA KUCHUKUWA FOMU YA URAIS KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VEIW MIGOMBANI ZANZIBAR.




MAMBO YA MASUALI KWA WAANDISHI WA HABARI KUWAULIZA WAGOMBEA NAE SALMA SAID WA GAZETI LA MWANANCHI AKITUMIA NAFASI YAKE KUMUULIZA DK. BILAL.



MDAU WA HABARI DONISIA AKIULIZA SUALI KWA MGOMBEA NDANI YA UKUMBI WA ZANZIBAR OCEAN VEIW MIGOMBANI.



MUANDISHI WA HABARI MUANDAMIZI SALIM SAID SALIM AKIULIZA SUALI KWA MGOMBEA NINI ATAFANYA AKIPATA RIDHAA YA CHAMA CHAKE KUMTEUWA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR.



MUANDISHI WA HABARI WA KITUO CHA ITV NA REDIO ONE FARUOK KARIM AKIMUULIZA SUALI MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR MHE. MOHAMMED GHARIB BILAL WAKATI AKITOWA DHAMIRA YAKE YA KUCHUKUA FOMU




WANACHAMA WA CCM WAKIMSIKILIZA MGOMBEA URAIS MHE MOHAMMED GHARIB BILAL AKITOWA DHAMIRA YAKE YA KUCHUKUA FOMU KWA AJILI YA KUGOMBEA KUTEULIWA NA CCM KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR .2010.



WANANCHI NA WANACHAMA WA CCM WAKIMSIKILIZA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU MOHAMMED GHARIB BILAL AKITOWA DHAMIRA YAKE YA KUCHUKUWA FOMU YA URAIS WA ZANZIBAR KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VEIW MIGOMBANI.



WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI WAKIMSIKILIZA MGOMBEA WA URAIS WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU DK. MOHAMMED GHARIB BILAL BAADA YA KUCHUKUA FOMU HIYO.

1 comment:

  1. Kinachonishangaza kidogo katika picha hizi mbona Vijana siwaoni?

    Naona wapambe wote na wasindikizaji ni wenye umri wa vijana wa zamani.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.