Habari za Punde

NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI MOHAMMED ABOUD MOHAMMED ACHUKUWA FOMU YA URAIS


Zanzibar Inaweza Kuwa Singapore Ya Pili - Aboud
Asema Hakuna Sababu Z’bar Kuwa Nyuma Kimaendeleo
lUvuvi wa bahari kuu, utalii nyenzo muhimu kufikia kujitegemea
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia CCM katika uchaguzi mkuu ujao, Mohammed Aboud Mohammed ameahidi kujenga ushindani wa maendeleo kati ya Zanzibar na visiwa vingine kama vile Singapore.
Amesema mazingira ya Zanzibar na Singapore yanalingana na kwamba hakuna sababu ya Zanzibar kuwa nyuma kimaendeleo tofauti na kisiwa hicho.
‘’Maendeleo ya Singapore na visiwa vingine ni mazuri hakuna sababu na sisi tusipige hatua ya maendeleo," alisema Aboud
Alisema kinachohitajika ni ubunifu na kutumia rasilimali ziliopo ili kufikia hatua kubwa kimaendeleo kwa faida ya taifa na wananchi kwa jumla.
Alifahamisha kwamba moja ya rasilimali hizo ni vivutio vya utalii Zanzibar ambavyo vinauwezo mkubwa wa kuibadilisha Zanzibar.
Pamoja na utalii, Aboud alisema bahari ya Zanzibar ina samaki wa kutosha na kwamba ikiwa kipaumbele kitawekwa katika uvuvi wa bahari kuu tunaweza kuanzisha viwanda vya kusindika samaki.
Kuhusu michezo, alisema Zanzibar inasifa ya kuwa na wanamichezo wazuri na kwamba endapo atashinda serikali itajenga chuo cha kufundisha michezo mbali mbali ili kulinda sifa hiyo.
MGOMBEA AKITOKA AFISI KUU YA CCM BAADA YA KUCHUKUWA FOMU.AKISALIMIANA NA WAPAMBE WAKE WALIOMSHINDIKIZA KUCHUA FOMU.
NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI MOHAMMED ABUOD MOHAMMED AKIPOKEA FOMU YA URAIS KUTOKA KWA KATIBU KAMATI MAALUM NEC ITIKADI NA UENEZI.
WAPAMBE WAKISHUHUDIA MHE. MOHAMMED ABUOD MOHAMMED AKLIKABIDHIWA FOMU YA URAIS AFISI KUU YA CCM KISUWADUI.
NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI MHE. MOHAMMED ABUOD MOHAMMED AKIMSIKILIZA KATIBU KAMATI MAALUM YA NEC NA ITIKADI NA UENEZE ZANZIBAR VUAI ALI VUAI BAADA YA KUIKAGUWA KADI YAKE YA CHAMA.
MHE MOHAMMED ABOUD MOHAMMED AKITOWA DHAMIRA YAKE KWA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUCHUKUWA FOMU AKIWA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA AL JOHARI SHANGANI ZANZIBAR.

NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI MOHAMMED ABOUD MOHAMMED AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI WA KITUO CHA TBC1 BAADA YA KUMALIZA KUTOWA DHAMIRA YAKE YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CCM.

MDAU WA HABARI WA KITUO CHA STAR TV PANDU ABDALLA AKITOWA SUALI KWA MGOMBE WA URAIS MHE. MOHAMMED ABOUD MOHAMMED KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA AL JOHARI BAADA YA KUCHUKUWA FOMU.
WADAU WA HABARI WALIKUWA NA UWANJA WA KUULIZA MASWALI KWA WAGOMBEA DHAMIRA YAO YA KUWANIA NAFASI HIYO.
MWANDISHI WA IDARA YA HABARI MAELEZO AJUZA JUMA AKIULIZA SUALI KWA MGOMBEA KUHUSIANA NA AZMA YAKE IKIWA ATATEULIWA NA CHAMA CHAKE KUGOMBEA URAIS ATAFANYA JIPYA GANI.
MWANDISHI WA REDIO ONE NA ITV MAULID HAMADI MAULID AKIMTWANGA SWALI MGOMBEA MHE. MOHAMMED ABOUD MOHAMMED KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA AL JOHARI SHANGANI.
WAANDISHI WAKIWA NA UCHU WA MASUALI KWA MGOMBEA MHE. MOHAMMED ABOUD MOHAMMED.

WAANDISHI WA HABARI WAKIMSIKILIZA MGOMBEA URAIS KUTEULIWA NA CCM KUGOMBEA NAFASI HIYO MHE MOHAMMED ABOUD MOHAMMED AKITOA DHAMIRA YAKE KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA AL JOHARI SHANGANI.
WANANCHI WAKIMSIKILIZA NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI MOHAMMED ABUOD MOHAMMED AKITOWA DHAMIRA YAKE KWA WANANCHI NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA AL-JOHARI SHANGANI ZANZIBAR.

3 comments:

  1. Mzee Mapara,

    Asante sana kwa hizi picha. Lakini vipi mbona ya Mh Mohd Aboud haipo? au uliishiwa na mkanda? Au kuna neno? Hebu tuekee hili hambo sawa.
    Mdau

    ReplyDelete
  2. Samahani si kama mkanda ulikwisha ila hatukupata angle nzuri ya kuweka potrait.

    Hata hivyo picha nyengine zinamuonesha mheshimiwa katika kujitasmbulisha na kujieleza kwa waandishi.

    Hakuna neno mdau ni katika kuwakilisha tu

    ReplyDelete
  3. Shukran sana Mzee Mapara. Nakupa hai kwa kazi yako kubwa ya kutumwagia hizi picha quality. Keep it up!
    Mdau
    USA

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.