Aahidi Kutumia Haki Katiba Na Sheria
Asema Busara Hekima Ndio Dira Yake
Zanzibar Itegemee Maendeleo Zaidi
CCM Ijipange Kwa Ushindi Uchaguzi Mkuu.
Bilal, Nahodha Wampongeza
Akizungumza mara tu baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Dk. Shein alisema yeye pamoja na wenzake watatumia hekima kubwa kwa kushirikiana, kuleta umoja na mshikamano ili CCM ipate ushindi.
Aidha aliwataka viongozi wenzake kuongoza kwa haki na sheria na kuachana na mambo yote yanayokwenda kinyume na sheria.
Aliahidi kuwa CCM itakuwa nguzo kubwa katika kukinadi na kukitangaza Chama Cha Mapinduzi huku akitekeleza majukumu kwa mujibu wa Ilani ya chama hicho.
Aliwahakikisha wananchi kuwa Zanzibar itapata maendeleo na kuongeza kuwa atafanya kazi bega kwa bega na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Muhammed Gharib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha waliokuwa pamoja katika tatu bora walimpongeza Dk. Shein kwa ushindi huo.
Asema Busara Hekima Ndio Dira Yake
Zanzibar Itegemee Maendeleo Zaidi
CCM Ijipange Kwa Ushindi Uchaguzi Mkuu.
Bilal, Nahodha Wampongeza
Akizungumza mara tu baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Dk. Shein alisema yeye pamoja na wenzake watatumia hekima kubwa kwa kushirikiana, kuleta umoja na mshikamano ili CCM ipate ushindi.
Aidha aliwataka viongozi wenzake kuongoza kwa haki na sheria na kuachana na mambo yote yanayokwenda kinyume na sheria.
Aliahidi kuwa CCM itakuwa nguzo kubwa katika kukinadi na kukitangaza Chama Cha Mapinduzi huku akitekeleza majukumu kwa mujibu wa Ilani ya chama hicho.
Aliwahakikisha wananchi kuwa Zanzibar itapata maendeleo na kuongeza kuwa atafanya kazi bega kwa bega na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Muhammed Gharib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha waliokuwa pamoja katika tatu bora walimpongeza Dk. Shein kwa ushindi huo.
Walioshindwa Waahidi Kumuunga Mkono
Homa Yahamia Kwa Mgombea Mwenza
Kupatikana Katika Mkutano Mkuu Kesho
Na Ramadhan Makame, Dodoma
Homa Yahamia Kwa Mgombea Mwenza
Kupatikana Katika Mkutano Mkuu Kesho
Na Ramadhan Makame, Dodoma
HATIMAYE kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kimemaliza uchakachuaji wa kumpata mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kulitangaza jina la Dk. Ali Mohammed Shein. kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Jina la mgombea huyo lilitolewa majira ya saa Nne usiku na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Taifa, Kepteni Mstaafu John Chiligati, baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Aidha mkutano huo ulimpitisha Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea pekee wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, baada ya Kikwete ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa sasa na Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa mwanachama pekee aliyejitokeza kuomba nafasi hiyo.
Chiligati alisema Dk. Ali Mohammed Shein alishinda kinyang’anyiro hicho baada ya kupata kura.117 ambazo zilitosheleza kuwashinda wenziwe Dk. Mohammed Gharib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha. ambao nao walikuwa wakiwania tiketi hiyo.
Katika mchuano huo Dk Mohammed Gharib Bilal alipata kura 54 na kumshinda Shamsi Vuai Nahodha aliyeshika mkia katika tatu bora kwa kupata jumla ya kura 33.
Majina hayo matatu ndiyo yaliyotarajiwa na wengi kutolewa kwenye kikao cha kamati hiyo, kwani ndio waliokuwa wakionekana kuwa na nguvu zaidi ikilinganishwa na wagombea wengine.
Awali kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu, majira ya saa tano jana kulikuwa na kikao cha kamati kuu ya CCM, ambayo ilipokea majina 11 ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar na kuyajadili kwa kina kila moja, na baadae kupitia majina matano yaliyopendekezwa na Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kuwania Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CCM.
Majina yaliyopokelewa na kamati hiyo kuwa tano bora ni pamoja na Haroun Ali Suleiman, Shamsi Vuai Nahodha, Dk. Ali Mohammed Shein, Ali Juma Shamuhuna na Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Kikao hicho kiliyachuja na kutoa majina matatu yaliyopelekwa Halmashauri kuu ambayo ilimpigia kura ... kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho na kupewa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu, ikiwa kikao hicho ndio cha mwisho kwa utaratibu wa CCM.
Kupatikana kwa jina la mshindi kwenye mchakato huo wa kumpata Rais wa Zanzibar kupitia CCM kumshusha presha kwa wananchi wa Zanzibar ambao kwa siku kadhaa sasa wamekuwa na hamu kubwa ya kumjua nani atakayekirithi kiti cha Dk. Amani Abeid Karume.
Hali hiyo inathibitika kutokana na Wazanzibari wengi ndio waliokuwa wakilizunguka jengo la Makao Makuu ya CCM Dodoma kwa zaidi ya wiki moja kabla ya kuhitimika kwa mchakato huo.
Siku mbili kabla ya kupitishwa kwa jina la Dk. Shein. kuwa mgombea wa urais mambo kadhaa yalizushwa ikiwemo Dk. Ali Mohammed Shein kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Pia ujio wa Rais Mstaafu Dk. Salmin Amuor Juma ambaye alipanda ndege moja na Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha nao ulitafsiriwa kuwa kiongozi huyo mstaafu amejiunga na kambi ya mgombea huyo.
Aidha makada hao walioingia tatu bora kambi zao zilipiga kampeni ya jino kwa jino mtu kwa mtu usiku na mchana ili kuhakikisha mgombea wao anaibuka na ushindi.
Wapambe hao walikuwa wakijinasibu mbele ya jengo la Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma kuwa mgombea wa upande wao ndiye atakayeshinda kutokana na kuwa na vigezo vyote.
Katika kujilabu kwao wapambe hao walikuwa na vigezo vinavyofanana katika kujinasibu huku wakiwasifia uwezo, zoefu na kuhimili mikikimikiki ya kwenye medani ya uongozi.
"Sisi hatuna wasiwasi sana tunajua mgombea wetu atashinda na kuiongoza Zanzibar, kwanza ana uzoefu anakubalika na ana kila sifa", alisema mmoja kati ya wapambe ambaye hakutaka mgombea wake wala yeye mwenyewe atajwe jina lake kabla ya kuibuka na ushindi.
Pia wapo waliokuwa wakidai wagombea wao ndio wenye kuweza kuiongoza Zanzibar kwani wanaelewa matatizo ya Zanzibar na wana uwezo wa kuyatatua.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Chama hicho Yussuf Makamba, alikaririwa akisema kuwa mchakato wa kumpata mgombea ulizingatia vigezo 11,hata hivyo katibu huyo alishindwa kuviweka hadharani.
Endapo miongoni mwa wagombea hao atashinda kwenye kinyang’anyiro hicho ya Urais kupitia chama cha Mapinduzi atakuwa rais wa awamu ya saba akimrithi Dk. Amani Abeid Karume anayemaliza muda wake kikatiba.
Zanzibar iliongozwa na awamu ya kwanza chini ya hayati Abeid Karume, akifuatiwa na Aboud Jumbe, mzee Ali Hassan Mwinyi, Idrisa Abdul Wakil, Dk. Salmin Amour Juma na Dk. Amani Abeid Karume.
Asubuhi ya jana karibu wagombea wote waliingia kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma wakipita kusalimia wajumbe waliofurika na wenye hamu ya kuwajua.
Miongoni mwa wagombea waliopita kwa mbwembwe ni pamoja na Haroun Ali Suleiman, Ali Juma Shamuhuna, Ali Abeid Karume, Shamsi Vuai Nahodha na Ali Mohammed Shein, huku wajumbe waliobakia hawakuonekana kujitokeza mbele ya wajumbe hao.
Hata hivyo wajumbe kama vile Hamad Bakari Mshindo, Omar Sheha Mussa na Mohammed Yussuf Mshamba walikuwepo kwenye jengo lililokuwa kikifanyika kikao cha kamati kuu.
Ni mgombea mmoja tu Mohammed Raza ambaye inaaminika hakuja kwenye mkutano huo ambapo hapo awali alidai kuwa hakupewa barua ya kuhudhuria kikao hicho cha mjini Dodoma.
Mgombea Haroun Ali Suleiman, baada ya kutopata nafasi ya tatu bora ameeleza kuwa ameridhika na maamuzi yaliyotolewa na Chama na ataunga mkono mgombea aliyewekwa na chama chake.
Kauli kama hiyo ya kuunga mkono pia ilitolewa na wagombea, Mohammed Aboud na Hamad Bakar Mshindo.
Nahodha nae kwa upande wake ameeleza kuwa makundi yote yamemalizika baada ya mchakato na wanaCCM wanaunda kundi moja na kupigania kwa nguvu moja chama chao kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa Zanzibar inahitaji kiongozi makini atakayeweza kukabiliana na changamoto za kimaendeleo kwa wananchi wa visiwa hivyo.
Mmoja kati ya wajumbe hao ambae hakutaka jina lake litajwe alisema aliwataka wanaCCM wavunje makundi yao na kujenga CCM imara ambayo itakwenda kushinda uchaguzi mkuu Oktoba ijayo.
“Mgombea amepatikana hatuna budi kumkubali na kuvunja makundi yetu, tujenge CCM imara tukijua kuwa tunakabiliwa na uchaguzi mkuu hapo baadae”,alisema mjumbe huyo.
Makada wa CCM walioomba nafasi ya kutaka kuwania urais kupitia chama hicho ni pamoja na Mohammed Raza, Hamad Bakari, Ali Juma Shamuhuna, Ali Abeid Karume, Dk. Ali Mohammed Shein, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mohammed Yussuf Mshamba, Shamsi Vuai Nahodha, Haroun Ali Suleiman na Omar Sheha Mussa.
Leo chama hicho cha CCM kinafanya mkutano mkuu wake utakaochukuwa siku mbili, ambapo Chiligati ameeleza kuwa utapitia ilani ya uchaguzi ya CCM kwa miaka 10 ijayo na kupiga kura ya NDIO na HAPANA kwa mgombea Urais wa Tanzania.
Aidha amesema Mgombea huyo atatangaza mgombea mwenza wake kesho katika mkutano huo mkuu.
Baada ya kumalizika kwa mchakato wa Urais wa Zanzibar, hofu ya Wazanzibari sasa imegeuka katika nafasi ya Mgombea Mwenza, ambae kwa mujibu wa Sheria atalazimika kutoka Zanzibar kwa vile Mgombea Urais ametoka Bara.Tayari kuna baadhi ya majina ya wanasiasa wa Zanzibar wakiwemo baadhi ya waliowania Urais wanatajwa kuwa ndio wataopewa nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment