Ali Mzee avipongeza vyombo vya habari kufanikisha kura ya maoni
Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Marekani imeipongeza Zanzibar kwa kuonesha kukomaa kidemokrasia, na kuamua kujenga Zanzibar mpya kufuatia kupiga kura ya maoni ya muundo mpya wa kisiasa kwa amani na utulivu Julai 31 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, alipozungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya watu sita ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Ali Mzee Ali, Afisi za Baraza hilo Mbweni Zanzibar jana.
"Nilipofika Zanzibar kwa mara ya kwanza, nilieleza hamu na matumaini yangu kwamba wananchi wa visiwa hivi vizuri wataungana na kujenga Zanzibar mpya iliyojaa amani.......nashukuru ndoto yangu hiyo imetimia muda mfupi sana" alisema Balozi huyo.
Balozi Lenhardt alieleza hatua hiyo ya viongozi na wananchi wa Zanzibar, imejenga historia ulimwenguni kote na kuichora Zanzibar katika ramani ya nchi zinazofuata demokrasia ya kweli.
Akizungumzia jengo jipya la Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Balozi Lenhardt alisema ni kiashirio kikubwa kwamba Wazanzibari wameamua kubadilika na kujenga Zanzibar mpya yenye mambo mapya ya kimaendeleo.
Kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010, Balozi huyo alisema una kila ishara ya kuwa wa mafanikio, huru na uliojaa amani, kama ilivyokwishaonekana kupevuka kwa wananchi wa Zanzibar, walipopiga kura ya maoni mwezi uliopita.
Alisema ni jambo la kufurahisha kuona Wazanzibari ndiyo wenye kufanya maamuzi kuhusiana na mustakbali wa nchi yao, pamoja na kushirikiana kuendesha nchi kwa pamoja baada ya uchaguzi mkuu na kuzifanya sauti za wananchi wote kusikilizwa, jambo ambalo Marekani na dunia nzima inalipongeza.

No comments:
Post a Comment